title : AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10
kiungo : AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10
AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
WATU wawili wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya Basi la Modern Coach lililokuwa likitokea nchini Kenya kuja Dar es salaam kupata ajali katika eneo la Mbwewe mkoani Pwani.
Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaeshi amethibitisha kupokea majeruhi hao leo saa 12 asubuhi.
Akizungumza na Michuzi Blog Aligaeshi amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti na majeruhi wote 10 ambao wamewapokea wanaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba gari iliyopata ajali jali basi hilo lilikuwa na abiria 45, dereva mmoja na tingo mmoja na abiria 43.
Wakati huo huo basi la Maning nice lililokuwa likitokea Dar kwenda Masasi limepata ajali baada ya kugonga basi la Tashrif kwa nyuma na kisha kugonga coaster 2.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo la Maning nice kuovatake eneo baya na kushindwa kurudi sehemu yake.
Shuhuda wa ajali hiyo ameeleza kuwa katika coaster hiyo, watu wengi wameumia.
Hivyo makala AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10
yaani makala yote AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/ajali-ya-basi-yaua-wawiliyajeruhi-10.html
0 Response to "AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10"
Post a Comment