title : ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI
kiungo : ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI
ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI
MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kupitia Chama cha ACT Wazalendo ametakiwa kujisalimisha katika kituo chochote cha Jeshi la Polisi nchini.
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ambapo amesema asipojisalimisha atasakwa kokote aliko.
Lugola amesema sababu za kumtaka Zitto kujisalimisha inatokana na kutoa kauli za uchochezi na kutoa lugha chafu dhidi ya viongozi wa nchini.
Amefafanua Zitto alitoa kauli hizo akiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Kilwa Abdallah Bunga maarufu kwa jina la Bwege.“Zitto ajisalimishe kituo cha Polisi Mkoa wa Lindi au kituo chochote cha Polisi nchini.Ametoa kauli hizo chafu kwenye jimbo ambalo kimsingi halimhusu.Hivyo amesema Lugola.
Pia ametoa agizo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro kuhakikisha anamchukulia hatua Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kilwa kwa kushindwa kumchukulia hatua Zitto akiwa katika wilaya hiyo.Wakati huo huo Lugola amewaonya wabunge wenye tabia ya kutoa lugha chafu na za uchochezi kwani hataacha hali hiyo ikaendelea na yoyote atakayethubutu atamchukulia hatua.
Amesema ni marufuku kwa mbunge yoyote kutoa lugha chafu, hata katika chaguzi ndogo zinazoendelea , uchaguzi wa mwakani na hata uchaguzi mkuu ujao.”Ni marufuku kwa mbunge yoyote kutoa lugha za uchechezi na katazo hili ni la mile na mile,”
Hivyo makala ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI
yaani makala yote ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/zitto-kabwe-apewa-siku-mbili-awe.html
0 Response to "ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI"
Post a Comment