title : WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA
kiungo : WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA
WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe (wa nne kutoka kushoto) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (kulia kwake) na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Brigedia Generali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri kupokea kivuko kipya cha MV. MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe (katikati) akikata utepe uliofungwa kwenye kivuko cha MV. MWANZA kuashiria kukamilika mapokezi ya kivuko hicho. Kivuko cha MV. Mwanza kimeanza kazi ya kubeba abiria na magari, mara baada ya mapokezi hayo kukamilika.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe (wa tano kutoka kushoto) pamoja na viongozi wengine wakishangilia kukamilika kwa zoezi la kupokea kivuko kipya cha MV. MWANZA. Kivuko cha MV. Mwanza kimeanza kazi ya kubeba abiria na magari, mara baada ya mapokezi hayo kukamilika.
Kivuko kipya cha MV. Mwanza kushoto kikiwa kimepaki katika maegesho ya Kigongo, kulia kwake ni kivuko cha MV. Misungwi ambavyo vyote kwa pamoja vina uwezo wa kubeba uzito wa tani 250, sawa na abiria 100 na magari 36 kwa wakati mmoja. Eneo la Kigongo/ Busisi sasa lina jumla ya vivuko vinne; MV. MWANZA, MV. MISUNGWI, MV. SENGEREMA pamoja na MV. SABASABA. Picha na THERESIA MWAMI - TEMESA
Hivyo makala WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA
yaani makala yote WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-kamwelwe-apokea-kivuko-cha-mv.html
0 Response to "WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA"
Post a Comment