title : WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI
kiungo : WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI
WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Jenista Mhagama, amefurahishwa na mwitikio wa waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) baada ya kuanza kushuhudia jinsi wafanyakazi wao wanavyonufaika na malipo ya Mafao ya Fidia.
Mhe. Waziri ameyasema hayo leo Julai 6, 2018 baada ya kutembelea banda la WCF kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere (Maarufu kama Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
“Nichukue fursa hii kuwashukuru waajiri wote nchini ambao wameitikia wito wa Serikali wa kujisajili na Mfuko kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. Nimetaarifiwa kuwa mpaka sasa jumla ya waajiri 14,855 wamesajiliwa na Mfuko. Na kinachonifurahisha zaidi ni kwamba sasa waajiri wameanza kuona manufaa ya kuanzishwa kwa Mfuko baada ya kushuhudia jinsi wafanyakazi wao wanavyonufaika na mafao yanayolipwa na Mfuko” Alisema Mhe. Waziri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, kwa mwaka wa fedha uliomalizika (2017/2018), tayari Mfuko ulikwishalipa mafao ya jumla ya shilingi bilioni 2.3 kwa wanufaika 812.” Alisema Bw. Mshomba.
Halikadhalika Bw. Mshomba alisema Mfuko umekuwa na faida sio tu kwa wafanyakazi na waajiri lakini pia hata kwa serikali kupitia kodi, ambapo alisema Mfuko umelipa kodi serikalini kiasi cha shilingi bilioni 3.2 kama kodi kwa mwaka wa 2016/2017 na mwaka huu ulioisha Juni 2018 tunatarajia kulipa zaidi ya shilingi bilioni 5 kama kodi ya serikali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kushoto), Naibu Waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji, Mhe. Eng. Stella Manyanya, (wakwanza kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba wakipatiwa maelezo na wataalamu wa Mfumo wa Kielektroniki wa Mfuko huo, Bw.Uforo Henry, (wapili kulia) na Abdi Kalilo wakati Mhe. Waziri na Naibu Waziri walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 6, 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kulia), akimuongoza Mhe. Waziri wakati akitembeela banda la Mfuko huo leo Julai 6, 2018.
. |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge (kulia) na mwenzake wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, wakibadilishana mawazo kwenye banda la WCF.
.
Afisa Uhusoano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Sebera Fulgence, (kushoto), akiwa na Justin Mwandumbya wa kitengo cha fedha
Maafisa wa WCF, Glady Madembwe, kutoka kitengo cha madai (Claims) (kushoto) na Afisa wa Afya na Usalama mahala pa kazi kutoka WCF, Bw. Robert Duguza (wapili kushoto), wakiwahudumia wananchi hawa waliotembelea banda la WCF.
Hivyo makala WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI
yaani makala yote WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-jenista-mhagama-aipongeza-wcf.html
0 Response to "WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI"
Post a Comment