title : WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA
kiungo : WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA
WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA
Na WAMJW Simiyu
Wananchi wa Kijiji cha Itindilo Wilaya ya Itimilo, Nangale na Migato vilivyopo Wilaya ya Itimila mkoani Simiyu wameungana kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuleta maendeleo kwa kuchangia nguvu kazi zenye thamani ya Shilling Millioni 24 kujenga Zahanati na kituo cha Afya vijiji hapo.
Hayo yamebainika wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akikagua huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii katika mkoa wa Simiyu.
Taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ikindilo imesema kuwa mradi huo unaogharimu jumla ya shilling 541,000,000 Shillingi 250,000,000 kutoka Serikalini, Shillingi Millioni 275,000,000 kutoka wadau wa Maendeleo UNFPA na Shillingi Millioni 16 kutokana na nguvu za wananchi.
Pia mradi ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha Nangale unaogharimu jumla ya shilling 36,321,000 Shillingi 30,000,000 kutoka Serikalini kwa kushirikiana na UNFPA, na Shillingi Millioni 6,321,000 kutokana na nguvu za wananchi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wanakijiji wa Migato na kuwahimiza kujitola katika kufanya shughli za kujiletea maendeleo wakati mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
Wananchi wa kijiji cha magito wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile( hayupo pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na mtoto mkaziwa Kijiji cha Migato mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA
yaani makala yote WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wananchi-wa-vijiji-vitatu-wilayani.html
0 Response to "WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA"
Post a Comment