title : WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI
kiungo : WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI
WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo kata ya jangwani mara baada ya kupewa zawadi ya gunia la mahindi na samaki wakati alipotembelea kwa ajili ya kuzungumza wananchi waliohamia ndani ya hifadhi ya Lipalamba iliyopo wilayani Nyasa moani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.
NA LUSUNGU HELELA- RUVUMA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Wakazi wa Kijiji cha Ndondo kata ya Jangwani wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamekiri mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kuwa wamevamia na wanaishi ndani ya eneo la hifadhi ya pori la akiba la Lipalamba lakini kwa kuwa hilo eneo wameshalizoea wanaiomba serikali kubadilishana nao na eneo jingine la kijiji lenye ukubwa sawa na eneo hilo walioingia ndani ya hifadhi hiyo.
Wananchi hao wametoa maombi hayo jana kwenye kwenye mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri huyo alioambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyasa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kwenye ziara ya siku tatu ambayo Naibu Waziri huyo aliifanya ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji wenzake, Pancrease Ndunguru alisema kuwa mpaka unaotenganisha kati ya kijiji na pori hilo ni mto unaojulikana kwa jina Tanginyama lakini wao wamejikuta wamevamia eneo hilo kwa kuanzisha makazi hivyo wanaomba hiyo sehemu waendelee kuishi lakini wakubali kubadilishana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo waliovamia Pori Akiba la Lipalamba iliyopo wilayani Nyasa moani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.
‘’Hili eneo sisi tushalizoea tunaiomba serikali ikubali ombi letu la kuweza kubadilishana na eneo lingine nje ya ukubwa sawa na eneo hili Alisema Pancreance Ndunguru. Naye, Diwani wa eneo hilo Ditram Nchimbi alimsihi Naibu Waziri alifanyie kazi ombi hilo la wanakijii kwa vile wameonesha uungwana kwa kutambua kuwa wamevamia baadhi ya eneo katika hifadhi ya Lipalamba lakini kitendo cha kukiri kosa ni uungwana wa hali ya juu hivyo walifanyie kazi ombi lao.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
Hivyo makala WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI
yaani makala yote WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wanakijiji-wakiri-mbele-ya-naibu-waziri.html
0 Response to "WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI"
Post a Comment