WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA

WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA
kiungo : WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA

soma pia


WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA




Wagombea 30 wa Udiwani katika uchaguzi Mdogo wa kata 77 utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu, wamepita bila kupingwa.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia amesema kuwa wagombea hao wamepita bila kupingwa baada ya Tume kukutana, kujadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi mbalimbali yaliyoweka na wagombea wa udiwani.

Amesema Madiwani wote waliopita bila kupingwa wanatoka Chama cha Mapindizi (CCM) na kuongeza kuwa rufaa zilipokelewa na kujadiliwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.

“Tume, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa 25 ambapo jumla ya wagombea kumi (10) walifanikiwa na hivyo kuendelea na uchaguzi na wagombea 15 rufaa zao hazikufanikiwa na hivyo kutoendelea kuwa wagombea,” amesema Dkt. Kihamia.

Ameongeza kuwa katika kata sabini na saba (77) wanachama 254 kutoka vyama kumi na moja (11) vya siasa walichukua fomu za uteuzi na kwamba jumla ya wanachama 186 sawa na asilimia 73.2 ya waliochukua fomu za uteuzi walizirejesha na kuteuliwa kuwa wagombea ambapo kati yao wagombea 179 sawa na asilimia 96.2 ni wanaume na wagombea 7 sawa na asilimia 3.8 ni wanawake.

“Hadi muda wa mwisho wa uteuzi ulipofika (saa 10.00 jioni siku ya uteuzi) wanachama 68 sawa na asilimia 26.8 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutorudisha fomu, kurudisha fomu nje ya muda unaokubalika kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo,” amesema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>>


Hivyo makala WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA

yaani makala yote WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wagombea-udiwani-kata-30-wapita-bila_82.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA"

Post a Comment