UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI

UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI
kiungo : UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI

soma pia


UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI

Na Ripota wetu, Globu ya Jamii
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe leo amefanya ziara ya mafunzo na ukaguzi wa Jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha  kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara hiyo Waziri Kamwelwe amesema amefurahishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kwamba anaamini akifika kwa awamu ya pili mambo yatakua mazuri zaidi. Amesema kuwa kufikia mwakani mwezi mei abiria wataanza kutumia uwanja wa Terminal 3.

"Nimefurahishwa sana na hatua ambayo ujenzi umefikia, kiwanja hiki kimejengwa kwa ubora wa kimataifa na miundombinu pamoja na vifaa vitatakavyo tumika katika jengo hili vitakua ni vya kisasa zaidi ambavyo viwanja vyote vya kimataifa hutumia", alisema Waziri Kamwelwe.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha JNIA Mhandisi Paul Rwegasha ameeleza kuwa kukamilika kwa jengo la tatu la abiria kunakuja na faida nyingi za kiuchumi kwa Taifa na mwananchi mmoja mmoja.

"Ukamilishwaji wa jengo hili la tatu la abiria katika Kiwanja Cha Kimataifa cha Julius Nyerere kutafungua milango mingi ya kiuchumi, serikali itaweza kupata mapato kupitia kodi za huduma mbalimbali zitakazo tolewa katika jengo hili, wananchi watapata ajira, wawekezaji wataongezeka na watalii pia", alisema Bwana Rwegasha.

Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha JNIA ameweka wazi kwamba, tayari mchakato wa kumpata mzabuni kwa ajili ya maandalizi ya kuhamia katika jengo la tatu la abiria na wazabuni kwa ajili ya upangaji wa maeneo ya huduma zitakazo patikana ndani ya jengo unaendelea.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe akizungumza na viongozi wanaosimamia mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati wa ziara yake aliyoifanya uwanjani hapo leo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA), Paul Rwegasha akizungumza kuhusu usimamzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Wolfgang Marschick akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria wakati wa ziara ya kwanza ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe akizungumza wakati alipokuwa anatembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kujionea ujenzi unavyoendelea.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe(wa pili kushoto) wakazi wa ziara ya kutembelea  mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI

yaani makala yote UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/uwanja-wa-ndege-wa-terminal-iii-kuanza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI"

Post a Comment