title : UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO
kiungo : UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO
UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini.
UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila Leseni ,Umri wa kuendesha gari kupitiliza , wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.
Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu Operesheni kikosi cha usalama Barabarani ,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi.
Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku baadhi ya Madereva wakikutwa na silaha katika magari yao vikiwemo Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .
Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo.



Hivyo makala UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO
yaani makala yote UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/ukaguzi-wa-magari-kilimanjaro-wabaini.html
0 Response to "UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO"
Post a Comment