TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka

TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka
kiungo : TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka

soma pia


TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka

 
 
*Yasema ni marufuku kufanya biashara pembezoni mwa reli, yaiomba jamii kulinda miundombinu

SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC)limesema linaendelea na mkakati wa uboreshaji wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka ambapo dola za Marekani milioni 300 zitatumika katika uboreshaji huo.

Limesema lengo la kuboresha reli hiyo ni muendelezo wa kuhakikisha usafiri wa treni nchini unakuwa wa uhakika zaidi na hiyo itafungua fursa za kiuchumi hasa katika kipindi hiki cha  mchakato wa ujenzi wa viwanda nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa Uboreshaji wa reli ya kati Mhandisi Mlemba Singo akiwa katika banda la TRC lililopo kwenye maonesho ya bishara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

Amefafanua mradi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia na utatekelezwa na TRC katika kipindi cha muda wa miaka miwili kuanzia Juni mwaka huu hadi Juni mwaka 2020.

Amesema lengo la uboreshaji wa reli ya kati ni kutoa usafiri wa kuaminika na kukuza upatikanaji wa huduma bora nchini  na maboresho hayo yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mzigo toka tani 13.5 za uzito wa ekseli hadi tani 18.5.

Mhandisi Singo amesema maboresho hayo yataenda sambamba na kutandika upya njia za reli zenye uzani wa paundi 80 kwa urefu wa kilometa 312, kufanya ukarabati wa njia ya reli iliyosalia kwa urefu wa kilometa 658 na kufanya ukarabati wa makaravati na madaraja 442.

Pia kuboresha mfumo wa mawasiliano , kuboresha vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es Salaam ,Ilala na Bandari kavu ya Isaka.

Amesema kuwa katika maboresho hayo wamejipanga kuboresha na kuongeza kiwango cha ubebaji mizigo kwa miundombinu ya reli na madaraja na kuongeza mwendokasi wa treni kutoka kilometa 35 kwa saa hadi kufikia kilometa 70 kwa saa.

Ameongeza kupitia mradi huo TRC pia imetengeneza mpango endelevu wa matengenezo ya miundombinu ili kufanya njia ya huo kuwa wa uhakika na kuaminika.

“Kuimarika kwa usafiri wa reli kutapunguza gharama za matengenezo ya barabara na hivyo Serikali kuendeleza bajeti iliyookolewa kwenda kwenye huduma nyingine za kijamii.

Mhandisi Singo amesema lengo lao pia ni kupunguza gharama na muda wa usafiri wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi bandari kavu ya Isaka hadi kufikia saa 24 kutoka zaidi ya saa 36 ya sasa.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa TRC Jamila Mbarouk amewataka Watanzania kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu ya reli na kufafanua kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakiharibu miundombinu na kufanya hujuma ikiwamo ya kuiba kokoto.

Pia amesma ni marufuku kufanya biashara pembezoni mwa reli na kwamba anayateka kufanya biashara pembeni ya reli itawezekana pale tu atakapopata kibali maalumu.

Mbarouk amesema ni marufu kupitisha mifugo kwenye reli na kueleza dhamira ya TRC ni kuona wananchi wananufaka na mradi huo na hakuna madhara yanayoweza kutokea.


Hivyo makala TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka

yaani makala yote TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/trc-yaendelea-kuboresha-miundombinu-ya_2.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TRC Yaendelea Kuboresha Miundombinu Ya Reli Ya Kati Kutoka Dar Hadi Isaka"

Post a Comment