title : TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU
kiungo : TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU
TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU
BENKI ya Posta ( TPB) imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 200 kwa wanajeshi wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania( JWTZ) nchini ili kujiendeleza kiuchumi na kuboresha maisha yao baada ya kustaafu .
Akizungumzia mjini Arusha Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki hiyo Henry Jonathan amesema kuwa wametoa mikopo hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu tangu waanze kutoa mikopo.Kwani benki hiyo inaongoza kwa kutoa mikopo mingi kwa wastaafu ambayo inawasaidia kuinua hali ya maisha na kuanzisha miradi ya uzalishaji.
Amesema kwa Mkoa wa Arusha wenye jumla ya wastaafu 600 wametoa bilioni 13.7 za mikopo kwa wastaafu hao ambao ni wanufaika wakubwa wa fursa hiyo ya mikopo.“Kama unavyojua benki ya Posta inaongoza kwa kutoa mikopo kwa wastaafu ili kuboresha maisha yao na kuhamasisha uwekezaji wenye tija utakaoinua vipato vyao na jamii kwa ujumla,” amesema Mkurugenzi huyo
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanajeshi wastaafu unaofahamika kama MUWATA, Luteni Mstaafu Geofrey Wapalila amesema kuwa mikopo hiyo imewasaidia kufungua biashara na kuwa wajasiriamali hasa wanapoanza maisha uraiani hivyo kuendeleza maisha yao vizuri pia wameishukuru benki hiyo kwa kuwaamini.Pia ameiomba benki hiyo kutoa mikopo ya vifaa kwa wajasiriamali ili waweze kuzalisha kwani bado wana nguvu za kufanya shughuli za uzalishaji.
Naye mmoja wa Wastaafu hao Leonard Kilasi ameshauri wastaafu hao kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati ili mikopo hiyo iwe na tija na kusaidia maisha yao.
Hivyo makala TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU
yaani makala yote TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tpb-yatoa-mkopo-wa-shilingi-bilioni-200.html
0 Response to "TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU"
Post a Comment