title : TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM
kiungo : TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM
TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema jana amepokea Msaada wa jengo la Choo cha kisasa chenye matundu 10 kilichojengwa katika Shule ya Msingi Kivule na kampuni ya Mafuta ya Total.
Akipokea msaada Kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Total nchini, Tarik Moufaddal, Dc Mjema amesema kuwa Msaada huo utasaidia kwa sehemu kubwa ya wasichana ambao walikuwa wanapata tabu ya vyoo katika shule hiyo.
Amesema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 3000 kwa sasa wanaweza kukabiliana na changamoto ya vyoo kwa watoto wa kike kutokana na kuongezeka kwa matundu hayo 10 ,ambayo yameelekezwa maalumu kwa ajili ya watoto wa kike.
“kwetu sisi huu ni msaada mkubwa sana kutoka Total kwani choo hichi kimegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 33 za kitanzania na kampuni hii imeweza kutenga Zaidi ya Milioni 700 kwa ajili ya kusaidia sehemu mbalimbali Tanzania kwanii tayari wamejenga choo kama hiki katika shule ya msingi Yombo Dovya hivyyo sisi watu wa ilala tunaomba wasiache kutukimbia kwani bado tutaitaji msaada Zaidi ya huu”amesema Dc Mjema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Total nchini Tarik Moufaddal amesema kuwa kampuni yake inaona fahari kuwa karibu na jamii kwa kuona inatoa msaada kwa watoto ili waweze kuwa katika mazingira mazuri na afya bora.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na Wanfunzi wa Shule ya Msingi Kivule mara baada ya kupokea Msaada wa Choo Cha Matundu 10 chenye thamani ya Milioni 33
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal wakati wa kuzindua jiwe la Msingi wa choo hicho
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kuanza kutumika kwa choo hicho.
Hivyo makala TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM
yaani makala yote TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/total-yakabidhi-choo-kwa-dc-shule-ya.html
0 Response to "TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM"
Post a Comment