title : RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL
kiungo : RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL
RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
RAIS Dk.John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitaifa wa tamasha la maalum la Mwezi wa Urithi kuenzi utamaduni wa Mtanzania ambalo litafanyika nchini nzima kwa kuaza na Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala amesema Serikali kupitia wizara hiyo wameaandaa tamasha hilo ambalo linalenga kuenzi utamaduni na urithi wa Mtanzania na kwamba tamasha hilo linaitwa Urithi Festival ambalo litakuwa likifanyika kila fikapo Septemba ya kila mwaka kuanzia mwaka huu.
"Dhumuni la tamasha ni kuenzi na kunadi kiutalii hazina kubwa ya utamaduni ,mila na desturi za makabila yote nchini ambayo ni zaidi ya 128.Hatua hii inaenda sambasamba na juhudi za Serikali za kuongeza wigo wa mazao ya utalii nchini hususan kukuza matumizi endelevu ya malikale,kutangaza utamaduni , vyakula vya asili , michezo ya jadi na kazi za sanaa mbalimbali.
"Tamasha litaisaida pia kukuza utalii wa ndani na kuongeza wastani wa watalii wa kimataifa kukaa nchini , hatua itakayoleta matokeo chanya kwenye mapato yatokanayo na sekta ya utalii na malikale.Wadau wa mwezi wa Urithi wa Tanzania ni Watanzania wote chini na waliopo ughaibuni .
"Aidha tamasha linawalenga raia wa mataifa mengine wanaoishi Tanzania na watalii wa kimataifa na kwamba tamasha litawashirikisha wadau wote wa utalii,"amesema Dk.Kigwangala.
Kuhusu namna ya kushiriki Dk.Kingwangala amesema Urithi Festival itasheherekewa Septemba yote na kwamba tamasha litafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri ambapo patakuwepo na matukio mbalimbali yakiwamo maonesho ya ubunifu wa sanaa na tamaduni , kazi za wajasiriamali na wadau wa utalii.

Hivyo makala RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL
yaani makala yote RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/rais-magufuli-mgeni-rasmi-ufunguzi-wa.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL"
Post a Comment