title : Manispaa ya Ilala inadhimisha wiki ya unyonyeshaji Duniani
kiungo : Manispaa ya Ilala inadhimisha wiki ya unyonyeshaji Duniani
Manispaa ya Ilala inadhimisha wiki ya unyonyeshaji Duniani
Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt, Emily Lihawa akizungumza na waandishi wa Habari hivi karibuni kuelezea Manispaa ya Ilala inavyotoa huduma za afya, katika vituo vyake pamoja na zahanati (Picha na Heri Shaban)
Na Heri Shaban
Mwambawahabari
OFISI ya Mganga Mkuu Manispaa ya Ilala imesema Agosti Mosi hadi Agosti Saba Tanzania unaungana na nchi nyingine Duniani katika madhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya MAMA .
Hayo yalisemwa Dar es salaam Jana na Ofisa Lishe manispaa ya Ilala Frola Mgimba katika Wiki ya unyonyeshaji Duniania ambapo Manispaa ya Ilala inawakumbusha Wananchi wake ju ya umuhimu wa maziwa ya MAMA na mtoto .
"Agosti Mosi hadi Saba ni Wiki ya maadhimisho ya unyonyeshaji maziwa ya mama kwa manispaa ya Ilala tunahamasisha kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na kwenye jamii kupitia watoa huduma ngazi ya Jamii" alisema FROLA.
Frola alisema maadhimisho hayo yanatusisitiza umuhimu wa Kulinda kuendeleza na kusaidia
uzalishaji bora wa watoto ambapo alisema siku ya unyonyeshaji hutoa fursa maalumu kwa watu wote kuungana pamoja katika kukumbushana umuhimu wa kuendeleza na kuimalisha umuhimu wa unyonyeshaji,maziwa ya mama Kama njia bora zaidi ya kujenga AFYA ya mtoto kimwili,kiakili na kijamii.
Alisema maadhimisho ya wiki ya unyonyesha ina umuhimu mkubwa sana katika kuzuia aina zote za utopia mlo kwa Watoto.
Alisema maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ni utolewaji wa Elimu ngazi ya kujenga uelewa wa JAMII juu ya umuhimu wa unyoshaji na uzalishaji JAMII alisema"Frola
Alisema dhumuni lingine kuhusiana maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa umma kuhusiana na unyonyeshaji ni muhimu kwa kuwa unazuia utopia mlo kwa watoto .
Aidha alisema dhumuni lingine kuhamasisha Wanawake wote wajue umuhimu wa kunyonyesha Maziwa ya mama peke yake kwa muda wa miezi sita ya Mwanzo wa maisha YA mtoto Mara baada kuzaliwa ndio njia bora Salama ya kumpatia mtoto virutubisho vyote kwa ukuaji wa Maendeleo yake.
Pia alisema manispaa ya ilala imepanga kutoa elimu ya unyonyeshaji ya maziwa YA mama kwa kuimiza wakina mama kuanza kunyonyesha mtoto ndani ya saa moja ya MAMA wakati wa kujifungua kunyonyesha mtoto mara kwa mara kadri anavyoitaji kuendelea kunyosheshwa maziwa ya mama peke yake kadri anavyouitaji kuendelea kunyonya peke yake bila kumpatia kitu kingine hata maji katika miezi sita ya Mwanzo
Hivyo makala Manispaa ya Ilala inadhimisha wiki ya unyonyeshaji Duniani
yaani makala yote Manispaa ya Ilala inadhimisha wiki ya unyonyeshaji Duniani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Manispaa ya Ilala inadhimisha wiki ya unyonyeshaji Duniani mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/manispaa-ya-ilala-inadhimisha-wiki-ya.html
0 Response to "Manispaa ya Ilala inadhimisha wiki ya unyonyeshaji Duniani"
Post a Comment