title : MAMBO SASA ATUA KUTOKA JAPAN NA MBINU MPYA, KAELEZA JINSI ATAKAVYO BORESHA ULINZI
kiungo : MAMBO SASA ATUA KUTOKA JAPAN NA MBINU MPYA, KAELEZA JINSI ATAKAVYO BORESHA ULINZI
MAMBO SASA ATUA KUTOKA JAPAN NA MBINU MPYA, KAELEZA JINSI ATAKAVYO BORESHA ULINZI
Mwamba wa habari
Na John Luhende
Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameagiza makamanda wote wa mikoa katika kanda hiyo kuhakikisha wanafufua vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na uhalifu.
Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameagiza makamanda wote wa mikoa katika kanda hiyo kuhakikisha wanafufua vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na uhalifu.
Pia amesema, yuko katika hatua za kuhakikisha Chanika inapewa hadhi ya kuwa Wilaya ya kipolisi sambamba na Jimbo la Kawe ambalo litakatwa na kuzaa wlaya nyingine ya Kipolisi ya Bunju.
Ameyasema hayo Dar es Salaam,leo wakati akihutubia katika kongamano la kudhibiti uhalifu katika jimbo la Ukonga.
Kamanda Mambo sasa amesema ni siku chache ametua nchini akitokea mafunzoni katika jiji la Tokyo nchini Japani ambapo ametua na mbinu mpya za kiusalama ikiwemo ya kuendesha vikundi vya ulinzi shirikishi.
Amesema, akiwa nchini Japan, alibaini wamefanikwa katika suala la ulinzi kwa kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo huko vinafahamika kama Coban na kwamba falsafa hiyo inatakiwa kutumika jijini Dar es Salaam.
“Naagiza makamanda wote wa polisi, kusimamia kikamilifu vikundi hivi.Polisi tutatoa mafunzo ingawa vikundi hivi vitakuwa chini ya viongozi wa mitaa yao,”alisema Kamanda Mambosasa.
Alisema,mafunzo haya kwa vikundi hivyo yataanza maramoja na kwamba amerudi na nguvu mpya ya kupambana na uhalifu kutoka nchini Japan.
Akizungumzia kuhusu biashara halamu ya dawa za kulevya, Kamanda Mambosasa alisema, eneo la Ukonga liko katika orodha hivyo changamoto hiyo pamoja na zingine zinamlazimu kuwa na Wilaya Maalumu ya Kipolisi ya Chanika.
“Pia wapo askari wachache ambao si waaminifu.Anapo mkamata mtu anazungusha kumpa dhamana ili mradi tu apewe chochote, Ninapokwenda kufufua ulinzi huu shirikishi ni lazima askari tujitafakari.Je tunatekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria, kanun na taratibu?”alihoji Kamanda Mambosasa.
Aliongeza; “Mimi ninavyoongea ndivyo nilivyo.Tupo kwaajili ya kuondoa kero za wananchi na si kutengeneza kero, hivyo wananchi tupeni kero hizo,”alisema Kamanda huyo.
Hivyo makala MAMBO SASA ATUA KUTOKA JAPAN NA MBINU MPYA, KAELEZA JINSI ATAKAVYO BORESHA ULINZI
yaani makala yote MAMBO SASA ATUA KUTOKA JAPAN NA MBINU MPYA, KAELEZA JINSI ATAKAVYO BORESHA ULINZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAMBO SASA ATUA KUTOKA JAPAN NA MBINU MPYA, KAELEZA JINSI ATAKAVYO BORESHA ULINZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mambo-sasa-atua-kutoka-japan-na-mbinu.html
0 Response to "MAMBO SASA ATUA KUTOKA JAPAN NA MBINU MPYA, KAELEZA JINSI ATAKAVYO BORESHA ULINZI"
Post a Comment