title : KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI
kiungo : KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI
KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI
Dr. N. T. Jiwaji
ntjiwaji at yahoo dot com
Usiku wa Ijumaa ya tarehe 17 Julai 1016 siyo wa kukosa kuangangalia angani. Usiku huo, Mwezi mpevu utafunikwa kabisa na kivuli cha Dunia na kusababisha kupatwa kamilifu na kuonekana wa rangi nyekundu. Kupatwa kunatokea wakati Dunia na Mwezi zinakuwa katika mstari mnyoofu, Dunia ikiwa kati ya Jua na Mwezi. Kupatwa huku kutukuwa wa kukolea sana na wa muda mrefu zaidi kwa karne hii.
Mwezi utafunikwa kwa muda mrefu zaidi kwa vile utakuwa na umbali mkubwa zaidi kutoka Duniani hivyo utapita ndani ya sehemu pana zaidi ya kivuli cha Dunia, na kuchukua muda mrefu zaidi kuvuka kivuli hicho. Safari hii Mwezi utabaki umepatwa kwa muda wa saa moja na dakika arobaini na tatu ambayo ni karibu masaa mawili hivi. Kupatwa kurefu kiasi hiki ni nadra sana kwa vilie kawaida ni dakika mia tu, kwa wastani. Kupatwa kurefu zaidi ya hii hakutatokea tena hadi baada ya miaka 105 ijayo siku ya tarehe 9 Juni, 2123.
Kupatwa kwa Mwezi kunaweza kuangaliwa kwa macho pekee bila madhara yoyote kwa vile tunafahamu kuwa mwanga wa Mwezi kawaida hautudhuru, na siku ya kupatwa mwanga unafifia hata zaidi baada ya kuzuiliwa na kivuli cha Dunia. Kupatwa kutaanza saa tatu na dakika ishirini na nne (3:24usiku) kwa kupatwa kiasi na kuanza kumegwa kingo ya mashariki ya Mwezi kwa kufunikwa na giza nyeusi ambayo itafunika Mwezi polepole hadi kufunika wote saa nne na nusu (4:30usiku), wakati ambapo Mwezi utakuwa umepatwa kamilifu na utageuka kuwa na rangi nyekundu. Hali hii ya Mwezi kuwa mwekundu wakati wa kupatwa kamilifu kutaendelea hadi saa sita na dakia kumi na tatu (6:13usiku) ambapo kupatwa kamilifu kutamalizika. Baada ya hapo kingo ya mshariku ya Mwezi itaanza kuchomoza kutoka katika kivuli na kuanza kuonesha uweupe utaongezeka polepole hadi saa saba na dakika kumi na tisa (7:19usiku) ambapo Mwezi utakuwa umeachwa na giza nyeusi, na ndio mwisho wa kukpatwa kiasi.
Pamoja na kuuona Mwezi ukiwa umepatwa kwa giza nyeusi, kuna sehemu ya kupatwa ambayo hatuwezi kutambua kwa urahisi. Wakati huo Mwezi unakuwa umefunikwa na kivuli chepsi cha Dunia. Hali hii ya kupatwa kwepesi itaanza saa mbili na dakika kumi na nne (2:14usiku) hadi saa tatu na dakika ishirini na nne (3:24usiku) ambayo ni mwanzo wa kupatwa kiasi na kuanza kuonesha giza ukingoni mwa Mwezi. Mwishoni tena kuna kupatwa kwepesi kuanzia mwisho wa kupatwa kisai saa saba na dakika kumi na tisa (07:19usiku) hadi saa nane na dakika ishirini na nane (08:28usiku) ambayo ndiyo mwisho kabisa wa tukio hili la kupatwa kwa Mwezi.
Ingawa Mwezi wote unamezwa ndani ya kivuli cha Dunia wakati wa kupatwa kamilifu, Mwezi haupotei moja kwa moja kwa vile mwanga kidogo hupenya ndani ya kivuli cheusi baada ya kupindwa na angahewa ya Dunia. Mwanga huu huwa ni wa rangi nyekundu na kusababisha Mwezi kuonekana kuwa wa rangi nyekundu muda wote ambao umepatwa kamilifu kuanzia saa 04:30usiku hadi saa 06:13usiku. Mandhari hii ya uwekundu wa Mwezi si wa kukosa kuuona kwa sababu kukolea kiasi hiki cha kupatwa kamilifu hakutatokea kwa miaka saba ijayo hadi Septemba 7, 2025
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI
yaani makala yote KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kupatwa-kamilifu-na-kurefu-zaidi-kwa.html
0 Response to "KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI"
Post a Comment