title : KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA
kiungo : KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA
KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Asas Dairies Ltd imeweka kitengo maalumu cha kuhudumia wateja wakubwa na taasisi(Corporate Sales Department) kwa lengo la kuhudumia wateja wao wanaofika kwenye banda lao katika Maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Matukio wa Kampuni ya Asas Jimmy Kiwelu amesema hayo leo wakati anazungumzia huduma mbalimbali ambazo wanazitoa kwenye maonesho hayo ambapo wameamua kuweka eneo maalumu kwa ajili ya kufanya mazungumza na wateja wakubwa na taasisi.
“Tumeamua kuweka kitengo maalumu cha Corporate Sales Department ambacho kazi yake ni kuwahudumia wateja wakubwa na taasisi.Lengo letu ni kuwahudumia wateja wetu wote ambao wanafika kwenye banda letu,”amesema Kiwelu.
Pia amesema wameweka eneo maalumu kwa ajili ya michezo ya watoto kwani wanatambua kuwa watoto baada ya kunywa maziwa ya Asas wanahitaji kupata muda wa kufurahi kwa michezo ya aina mbalimbali.
“Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunawajengea watoto utamaduni wa kupenda kunywa maziwa.Kwa kupitia michezo iliyopo kwenye banda letu watoto watafurahi na wataendelea kukumbuka maziwa bora na halisi ya Asas,”amesema.
Kwa upande wa mmoja wa wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Sales Department Elizabeth Balele amesema kuwa kazi nyingine ya kitengo hicho ni kuilezea kampuni hiyo kwa wale ambao wanahitaji kuifahamu zaidi na hasa kuhusu bidhaa zake.
“Pia tunalo jukumu la kuwaelimisha wateja wakubwa ambao wanahitaji uwakala, kununua au kuuza ambao wanahitaji kuuza bidhaa zetu katika maeneo yao husika,”amesema.
Meneja wa Masoko na Matukio wa Kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelo akizungumza na Mdau wa Maendeleo mkoani Iringa Bw. Fredrick Mwakalebela wakati alipotembelea katika banda la kiwanda hicho kwenye maonesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Mmoja wa wafanyakazi wa kitengo hicho cha(Coperate Sales Department)Elizabeth Balele akiwa katika eneo lake la kazi tayari kwa kuhudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea katika banda la kiwanda hicho.
Mmoja wa wafanyakazi wa kitengo hicho cha(Coperate Sales Department)Elizabeth Balele akiwahudumia wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la kiwanda hicho.
Hivyo makala KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA
yaani makala yote KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kampuni-ya-asas-yaweka-kitengo.html
0 Response to "KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA"
Post a Comment