title : KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO
kiungo : KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche mara baada ya kuwasili Gereza la Wilaya Same kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia leo Julai 31, 2018, Mkoani Kilimanjaro kabla ya kuendelea na ukaguzi katika magereza ya mwanga na Gereza Rombo. Lengo la ziara hiyo ni kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiongea na Maafisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Same alipotembelea gereza hilo katika ziara yake ya kikazi leo Julai 31, 2018(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche.
Maafisa na askari wa Gereza Same wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza(hayupo pichani) alipotembelea gerezani hapo katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (wa kwanza kushoto) akikagua nyumba ya askari inayojengwa kwa njia ya kujitolea katika Gereza la Wilaya ya Same. Nyumba hiyo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi familia nne za askari hivyo kutatua uhaba wa nyumba katika gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Same alipotembelea gereza hilo kwa lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo Mkoani Kilimanjaro leo Julai 31, 2018(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).
Hivyo makala KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO
yaani makala yote KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kamishna-jenerali-wa-magereza-phaustine_31.html
0 Response to "KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO"
Post a Comment