title : HESLB yajipanga kuongeza ufanisi
kiungo : HESLB yajipanga kuongeza ufanisi
HESLB yajipanga kuongeza ufanisi
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema wameyapokea maoni ya wadau na watayafanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika utoaji na urejeshaji wa mikopo.
Badru aliyasema hayo wakati akizungumza katika banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kwenye maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Amesema kuwa HESLB inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wazazi, wanafunzi pamoja wanufaika wa mikopo.
Amesema kuwa wadau wakifika katika banda la bodi watapata ufafanuzi wa vipengele kwa waombaji mikopo katika bodi hiyo utakaomalizika Julai 15 mwaka huu kwa waombaji hao kupata taarifa sahihi.Badru amesema kuwa wanufaika wa mikopo pia watapata elimu ya urejeshaji wa mikopo iliyoiva ili kuweza kurejesha katika mfuko kwa ajili wengine kunufaika ikiwa ni pamoja na kujua ankara zao kwa ajili ya kulipa kutokana na kuwepo na changamoto katika malipo.
Aidha amesema kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa na mwamko wa kukata asilimia 15 ya mshahara huku wengine wakikata bila kupeleka bodi kwa wakati muafaka.Amesema waajiri ambao wamekuwa wakishindwa kufanya malipo kwa wafanyakazi wao wamekuwa wakiwapeleka mahakamani na wakifika huko wanaomba wazungumze nje ya mahakama na matokeo yake wanalipa.
Badru amesema kuwa mikopo inatolewa kwa wenye mahitaji maalum na vipaumbele ikiwa kwa watoto yatima, kipato duni, wenye ulemavu na wale ambao wanasomea sekta ambazo zinahitaji wataalam katika kuziba nafasi za utalaam huo.“Changamoto kubwa tuliyonayo ni kuwa waombaji wengi hawasomi mwongozo tunaoutoa na hivyo wanakosea kujaza fomu za maombi mtandaoni. wito wetu kwao ni kuwa wausome kwa makini na kuuzingatia,” amesema Bw. Badru.
HESLB ilianzishwa kwa sheria mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na kukusanya mikopo iliyoiva ambayo imetolewa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam na kushauri HESLB ishirikishe wadau katika kutatua changamoto za urejeshaji mikopo iliyoiva.
Akizungumza katika banda la HESLB, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Prof. Joe Lugalla amesema wanufaika wengi wa mikopo ya elimu ya juu hawana ajira rasmi na hivyo kuhitajika ushirikishwaji mkubwa zaidi ili kuwafikia na kuongeza makusanyo.
“Kuna wanafunzi wengi wamemaliza masomo na wapo vijijini wanaendelea na shughuli zao binafsi…ni vizuri wadau mbalimbali kama taasisi za elimu ya juu zishirikishwe ili kuwabaini,” amesema Prof. Lugalla.
Naye Mussa Sayenda ambaye ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu na mhitimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema HESLB inapaswa kuboresha matumizi ya teknolojia kwa kuwa na mfumo unaomwezesha mnufaika kupata taarifa za deni lake popote alipo.
Kwa upande wake, Bi. Severine Mwakalukwa ambaye ni mlezi wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE) ameishauri HESLB kuboresha vigezo vya utoaji mikopo ili kuondoa malalamiko ya upangaji mikopo kutoka kwa baadhi ya wanafunzi.
01.Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akizungumza na Mwandishi wa Michuzi Blog katika banda la bodi hiyo katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akiwapa huduma wananchi waliotembelea banda la bodi katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Prof. Joe Lugalla akipata maelezo katika banda la bodi ya mikopo alipotembelea maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala HESLB yajipanga kuongeza ufanisi
yaani makala yote HESLB yajipanga kuongeza ufanisi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HESLB yajipanga kuongeza ufanisi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/heslb-yajipanga-kuongeza-ufanisi.html
0 Response to "HESLB yajipanga kuongeza ufanisi"
Post a Comment