title : HAFTRADE waomba shamba la kilimo darasa Handeni
kiungo : HAFTRADE waomba shamba la kilimo darasa Handeni
HAFTRADE waomba shamba la kilimo darasa Handeni
Diwani wa Kata ya Malezi Wilayani Handeni Mkoani Tanga.Shabani Kitombo akifungua kikao cha taasisi isiyo ya Serikali ya Handeni Mjini HAFTRADE inayoshugulika na shuguli za kijamii(kushoto)Mkurugenzi wa taasisi hiyo Teckla Mingwa (Picha na Heri Shaban )
wanachama wa Taasisi ya HAFTRADE wakiwa katika Picha ya pamoja Wilayani Handeni Mkoani Tanga jana Mara baada kumaliza kikao cha taasisi hiyo ,(PICHA NA HERI SHAABAN)
Na Heri Shaban,Tanga
Mwambawahabari
SHIRIKA lisilo la Kiserikali linaloshughulika na shuguli za Kijamii HAFTRADE limetuma maombi kwa Wanakijiji
Wilaya ya Handeni Mjini ili wapatiwe eneo la ekari 100 kwa ajili ya kilimo na Shamba darasa.
Akizungumza Handeni Mjini jana Mkurugenzi wa shirika la HAFTRADE Teckla Mingwa alisema taasisi yake imeomba eneo la ekari 70 ili litumike katika kilimo pamoja na shamba darasa lakini tunawashukuru wananchi tumekubaliwa kupewa zaidi ya ekari 100 alisema ".Mingwa
Mingwa alisema kamati iliyoteuliwa kushugulikia Jambo hilo imefanikiwa ipo katika hatua za mwisho na Wanakijiji.
Alisema taasisi hiyo inashughulika na shuguli za kijamii katika Kata tisa za Wilaya Handeni mjini kwa kuibua miradi ya wananchi ambapo kwa sasa imefanikiwa kujenga madarasa matatu eneo la kwamadule.
Mingwa alisema kwa sasa ujenzi wa madarasa matatu ya Shule ipo hatua ya kumaliza ujenzi ili aweze kuyakabidhi Serikali ya kijijini watoto wasome karibu na makazi yao.
Aliwataka wananchi wa wilaya hiyo,kushirikiana na taasisi hiyo kwa ajili ya kuleta Maendeleo.
"Shirika letu la HAFTRADE linashughulika na shuguli za kijamii ikiwemo kutatua kero za Elimu, AFYA, Mazingira na kero ya maji katika Kata tisa"alisema.
Kwa upande wake Mkandarasi Davidan Gen Suplies Com Ltd, ya Handeni Mjini Vicenti Daniel alisema kwa muda wa wiki moja atakuwa amemaliza ujenzi na kukabidhi madarasa hayo ..
Daniel alisema mafundi wake wameshaanza ujenzi wapo katika hatua za mwisho ili wakabidhi madarasa ya shule ya kijiji.
Alisema ujenzi wa madarasa hayo matatu alianza kujenga hivi karibuni baada kupewa tenda na Taasisi ya HAFTRADE yenye makazi yake Handeni mjini
Naye Diwani wa Kata ya Malezi Handeni Mjini
Shaban Kitombo alipongeza HAFTRADE kwa kutatua changamoto katika wilaya hiyo kwa kusaidiana na Serikali katika kufanikisha ujenzi wa madarasa Eneo kwamadule na miradi mingine ya Jamii.
Aliziomba taasisi zinginge kushirikiana na serikali katika kitatua kero na kuibua miradi mipya katika kata za Handeni mjini ambazo ni Chanika, Kideleko,Konje,Kwamagome,Kwediyamba,Kwenjugo Magharibi, Kwenjugo MASHARIKI, Mabanda, Malezi, Mlimani, Msasa na Vibaoni
Hivyo makala HAFTRADE waomba shamba la kilimo darasa Handeni
yaani makala yote HAFTRADE waomba shamba la kilimo darasa Handeni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAFTRADE waomba shamba la kilimo darasa Handeni mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/haftrade-waomba-shamba-la-kilimo-darasa.html
0 Response to "HAFTRADE waomba shamba la kilimo darasa Handeni"
Post a Comment