Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani

Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani
kiungo : Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani

soma pia


Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani


Mwamba wa habari
Mkurugenzi wa Kampuni ya Halihalisi inayochapisha magazeti ya Mawio, Mwanahalisi na Mseto, Saed Kubenea amesema watarudi Mahakama ya Afrika Mashariki kuomba kibali cha kuchapisha gazeti la Mseto baada ya Serikali kutoondoa zuio la uchapishaji.

Mahakama hiyo Juni 21, 2018 ilitoa amri kwa Serikali kuhakikisha inachukua hatua stahiki ili gazeti hilo lirudi mtaani ikisema lilifungwa kinyume cha sheria.

Gazeti hilo lilifungiwa Agosti 10, 2016 kwa miezi 36 ikielezwa ni kwa kuandika habari za upotoshaji, uchochezi na uongo, zisizozingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

 Kubenea akizungumza na waandishi wa habari  jana Jumapili Julai 22, 2018 alisema Serikali sasa inapaswa itoe ushirikianao kwa Mahakama ili usikilizaji wa kesi za madai na jinai ufanyike kwa haraka kuliko kucheleweshwa bila sababu za msingi.

"Tungekuwa tuna mitambo yetu tungekuwa tumechapisha tangu siku ambayo Mahakama imetengua agizo hilo lakini nashindwa kwa sababu wachapishaji wanahitaji hati ya usajili wa gazeti kabla ya kuchapishia,” alisema Kubenea.

“Lakini hicho kibali tutakachopewa na Mahakama kitatumika kama kigezo cha sisi kuchapisha na kuuza gazeti," aliongeza Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo (Chadema).

Wakili kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Fulgence Massawe amesema kitendo cha kuchelewa kutengua uamuzi wa kufungiwa kwa gazeti hilo ni ukiukaji wa sheria ambao unapaswa kuangaliwa.

"Siyo kwamba Serikali haina taarifa, siku hukumu inasomwa walikuwa na mawakili wa upande wa Serikali ambao walisikia na kuahidi kutekeleza maagizo," amesema Massawe na kuongeza:

“Serikali tayari imeandaa notisi ya rufaa kupinga hukumu hiyo na itaiwasilisha Jumatatu lakini jambo hilo halizuii kuanza kwa utekelezaji wa hukumu iliyotolewa,” amesema


Hivyo makala Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani

yaani makala yote Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/gazeti-la-mseto-kurudi-mahakamani.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Gazeti la Mseto Kurudi Mahakamani"

Post a Comment