CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA

CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA
kiungo : CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA

soma pia


CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA

Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo wakati alipotembelea maktaba ya shule ya sekondari Mboga ,aliyesimama ni mkuu wa shule ya sekondari ,George Mwakihaba.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (mwenye shati jeupe) akiangalia namna mwanafunzi wa shule ya sekondari Mboga akifanya mafunzo ya somo la sayansi kwa vitendo wakati alipotembelea maabara ya shule ya sekondari Mboga.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo wakati alipotembelea maktaba na maabara ya shule ya sekondari Mboga .(picha na Mwamvua Mwinyi).

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

SHULE 13 za sekondari, halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani ,zinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya maabara za masomo ya sayansi, ikiwa ni sawa na upungufu wa vyumba 39.

Afisa elimu sekondari Chalinze, Timothy Bernard aliyasema hayo ,wakati mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alipotembelea maabara zilizokamilika shule ya sekondari Mboga, ikiwa ni sehemu yake ya kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo jimboni humo. Alisema ,halmashauri hiyo ina jumla ya shule 17 za serikali ambapo shule nne zimeshakamilisha vyumba 12 vya maabara zinazotakiwa.

"lengo letu ni kuhakikisha tunatenga bajeti kila mwaka ili kujenga maabara hizo, awamu kwa awamu hadi hapo tutakapomaliza tatizo hilo ,na hatimae watoto wetu waendelee kunufaika na masomo ya sayansi kwa vitendo" alisema Bernard.

Mkuu wa shule ya sekondari Mboga, George Mwakihaba ,alimshukuru mbunge huyo ,wadau ,bank ya dunia, ,halmashauri na nguvu za wananchi kwa kujitoa kwao kukamilisha maabara zote shuleni hapo. Alisema miaka ya nyuma walikuwa na maabara moja pekee ,iliyotumika kwa masomo yote matatu ya sayansi, hali iliyokuwa ikisababisha wanafunzi kutofanya vizuri kwenye masomo ya mafunzo kwa vitendo.

Mwakihaba alielezea ,licha ya changamoto ya ukosefu wa maabara kubaki historia wanakabiliwa na ukosefu stuli na vifaa vya kuhifadhia kama makabati.

Nae Ridhiwani alisema kuwa ,viongozi wanapaswa kujenga tabia ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyokamilika na ambayo bado kukamilika ili kujiridhisha namna ya ujenzi unaofanyika. Alisema, maabara ya sekondari Mboga ina upungufu wa baadhi ya vifaa suala ambalo amelibeba na ataangalia namna ya kulisaidia .

Akizungumzia ziara yake kwenye miradi ya maendeleo ,Ridhiwani alieleza ,ametembelea kituo cha afya Msoga ,maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa unaojengwa Msoga, sekondari ya Mboga na kiwanda cha Sayona .


Hivyo makala CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA

yaani makala yote CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/chalinze-kutenga-bajeti-kila-mwaka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA"

Post a Comment