title : BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)
kiungo : BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)
BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario akizungumza katika warsha ya mafunzo ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kukuza ujuzi na uendeshaji wa biashara pamoja na misingi ya ulipaji kodi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara wakiwa wanafuatilia kongamano lililoandaliwa na Benki ya KCB lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Mkufunzi wa masuala ya Kodi Charles Adolf kutoka Adolf Tax Consul akizungumza na wafanyabiashara na kuwahimiza wapate elimu ya kodi ili kusaidia ongezeko la pato la taifa katika Kongamano lililoandaliwa na Benki ya KCB Leo Jijini Dar es Salaam
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya KCB Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira ya kuwaendeleza wafanya biashara wadogo na wa kati (SME) kwa kuendesha kongamano la pili kwa wafanya biashara zaidi ya 200 jijini Dar es Salaam.
Benki hiyo imeandaa Biashara Club ambayo ni mpango maalum unaowasaidia wafanya biashara kukuza ujuzi katika maswala ya fedha, uendeshaji wa biashara na kanuni na misingi ya kulipa kodi pamoja na kuwapa fursa za kukuza mahusiano yao na wafanya biashara wengine ndani na nje ya nchi.
Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Serena ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo. Nia kubwa na KCB Bank ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba.
Akiongea katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Bw. Cosmas Kimario, alisema “Hakuna biashara inayofanikiwa bila changamoto. Hizi zipo ili zikupe chachu, uzikabili, usonge mbele. Wanaokimbia changamoto huanguka kibiashara ama huendesha biashara zisizo endelevu.”
Katika ushauri wake alisisitiza kwamba namna pekee ya kuzikabili changamoto hizo ni “ubunifu, kujali muda, kwenda kwa wakati, kufahamu kanuni muhimu za nchi na za kisheria katika biashara.”
Mkufunzi wa masuala ya Kodi Charles Adolf kutoka Adolf Tax Consul aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muhimu wa kuelewa mfumo wa kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara biashara zao. “Hamna taifa linaloendelea bila kodi lakini pia ili kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi imara ni lazima tulipe kodi.”
Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua wigo wa biashara zao. KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.
Hivyo makala BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)
yaani makala yote BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME) mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/benki-ya-kcb-yadhamiria-kuwainua.html
0 Response to "BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)"
Post a Comment