YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO

YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO
kiungo : YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO

soma pia


YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO

Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

KUELEKEA Mkutano mkuu wa Yanga Juni 10 mwaka huu, uongozi umeweka wazi ajenda kuu zitakazojadiliwa huku ajenda ya uchaguzi ikiwa imewekwa kando kwanza.

Maandalizi ya mkutano huo kwa wanachama wa Klabu ya Yanga yameshika kasi sasa zikiwa zimesalia siku nne kuelekea mkutano huo muhimu utakaotoa dira kwa klabu hiyo.

Akielezea masuala mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wako hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa maofisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Mkwasa amesema wanakusudia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti na mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

"Tunatarajia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo Yusuph Manji ambaye alikua mwenyekiti na mfadhili wa klabu hii, Baraza la Michezo,TFF  pamoja na wizara husika,"amesema Mkwasa.

Mwaliko utapelekwa pia kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Moja ya ajenda katika Mkutano huo maalumu kwa wanachama ni kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo, ikiwa pamoja na suala zima la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Katika ajenda zingine zinazotarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kujadili ushiriki wa Yanga katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua waliyofika kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, Mapato na Matumizi, bila ya kusahau Mabadiliko kuhusu mfumo wa uendeshaji.

Pia katika suala la uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi huenda litawasilishwa kupitia mengineyo.Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa ajenda hiyo kuondolewa ili kuwapa nafasi wanachama kujadili masuala muhimu.

Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema mkutano huo utakuwa na lengo la kuwaeleza wanachama matatizo yanayoikabili timu yao, kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi zililizo wazi utatangazwa baadaye.


Hivyo makala YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO

yaani makala yote YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/yanga-waanika-ajenda-za-mkutano-mkuu-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO"

Post a Comment