Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme

Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme
kiungo : Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme

soma pia


Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme


Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiongozwa na Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati, wamekagua mradi wa umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika wilaya mbalimbali mkoani Tanga na kuzindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo, wilayani Korogwe.

Mhandisi Msembele, ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu katika uzinduzi huo, alisema kuwa, kuzinduliwa kwa huduma ya umeme katika Kijiji hicho kumewezesha wananchi zaidi ya 63 kuunganishwa na huduma ya umeme huku wateja 180 tayari wameshalipia huduma hiyo.

" Niwapongeze wananchi wa Kijiji hiki cha Bagamoyo kwa kuchangamkia huduma ya umeme, lakini niwakumbushe kuwa inapaswa kutumia umeme kwa ajili ya kufanya shughuli za kiuchumi kama kufunga mashine za kusaga nafaka na si kuwasha taa peke yake, " alisema Mhandisi Msembele.

Wataalam wengine walioambatana na Mhandisi Msembele ni  Afisa Upimaji kutoka REA, Hussein Shamdas, Meneja wa TANESCO mkoa wa Tanga,  Eng. Cecilia  Msangi na Meneja wa TANESCO, wilaya ya Korogwe, Julius Nyamarungu.

 Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakikagua transfoma zitakazotumika kusambaza umeme vijijini katika Wilaya ya Korogwe. Kushoto ni Hussein Shamdas kutoka REA na katikati ni Yusuph Msembele.
 Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati (wa Tatu kulia) akikata utepe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo wilayani Korogwe mkoa wa Tanga. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka TANESCO, REA na wawakilishi wa wananchi.
 Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati akibonyeza kitufe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo wilayani Korogwe mkoa wa Tanga. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka TANESCO, REA na wawakilishi wa wananchi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme

yaani makala yote Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wataalam-wizara-ya-nishati-rea-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme"

Post a Comment