WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA

WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA
kiungo : WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA

soma pia


WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA

MKUU wa wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, Bw. Juma Sweda amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanatumia vizuri fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya zao la pamba.
Amesema ni vema wakatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika familia zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba bora na za kisasa na wawaendelea watoto kielimu.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 11, 2018) wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za uvunaji na uuzaji wa zao la pamba. Ziara hiyo imefanyika kwenye vijiji vitatu vya kata ya Mondo wilayani hapa.

Bw. Sweda amesema wananchi wengi walihamasika kulima zao la pamba baada ya Serikali kuhamasisha walime na kuahidi kulifuatilia kuanzia hatua za utayarishaji wa mashamba hadi utafutaji wa masoko.

“Naishukuru Serikali kwani baada ya kuhamasisha ufufuaji wa kilimo cha zao la pamba nasi tuliungana na wananchi kuhakikisha maelekezo hayo tunayatekeleza kwa vitendo, lengo letu kubwa ni kuona zao hilo linarudi kama zamani,” amesema.

Amesema kwa sasa wapo katika hatua ya uvunaji na uuzaji, ambapo wamejipanga kukagua kikamilifu ili kuona zoezi hilo linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya Ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika.

Amesema viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) hukagua pamba kabla ya kuipokea na iwapo mkulima atabainika kupeleka pamba chafu hulazimika kuisafisha kwanza kwa kutenga safi na chafu ndipo hupima na kulipwa.
Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda (kushoto) akikagua shamba la pamba la Bw. Swalala Nteminyanda (kulia) katika kijiji cha Nyanh'onge wilayani humo  Juni 11, 2018. Ununuzi wa pamba  kwa pesa taslimu wilayani Misungwi unaendelea vizuri na kilo moja inanunuliwa kwa shillings 1100/=. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mkulima wa pamba katika kijiji cha  Mondo wilayani Misungwi, Hoja Ngole akitumia mkokoteni wa kokotwa na ng’ombe kupeleka pamba yake kuuza kwenye  Chama cha Ushirika  wa Mwaniko katika kijiji cha Mondo Juni 11, 2018. Uuzaji wa pamba wilayani Misungwi unaendelea vizuri na kilo moja inauzwa kwa sh. 1100/=.
  Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo, Philip Makoye akionyesha pamba cha aliyoikataa na kuamuru ichambuliwe tena na mkulima aliyetaka kuiuza katika chama hecho wilayani Misungwi, Juni 11, 2018.
 Wakulima wa zao la pamba Bibi Pendo Kitwala (katikati) na Sospeter Shija wakichambua pamba  iliyokataliwa baada ya kugundulika kuwa ni chafu wakati walipotaka kuiuzwa katika  Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo wilayani Misungwi Juni 11, 2011.  Ukaguzi  wa hali ya juu unafanyika  msimu huu wa uuzaji zao hilo ili kuwanasa wakulima wachache  wanaojaribu kuuza pamba chafu. Lengo la hatua hiyo ni  kurejesha heshima ya ubora na sifa nzuri ya pamba ya Tanzania katika soko la dunia. Kushoto ni   Mussa Daudi akiwasaidia wazee hao.
 Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo, Phillip Makoye (kushoto) akipima katika mzani pamba ya  Marco Masalamunda (watatu kulia) kwenye ghala la chama hicho cha msingi lililopo Katika jijini cha Mondo wilayani Misungwi Juni 11, 2018. Ununuzi wa zao la pamba kwa fedha taslimu unaendelea vizuri wilayani humo na kilo moja inanauliwa kwa shillingi 1100/=.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA

yaani makala yote WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wanamisungwi-tumieni-vizuri-fedha-za_11.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WANAMISUNGWI TUMIENI VIZURI FEDHA ZA PAMBA-DC SWEDA"

Post a Comment