WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA.

WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA.
kiungo : WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA.

soma pia


WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba

MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamempongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba kwa kuazisha utaratibu wa kuwajengea uwezo wananchi juu ya muhimu wa kutunza mazingira jambo ambalo wanaamini litasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira.

Wakizungumza na Mwamba wa habari blog wakazi hao wamesema kuwa kampeni ya mazingira itasaidia kuhamasisha watu kusafisha na kutunza mazingira kwa manufaa ya  pamoja na vizazi vijavyo.

Hamisi Jumanne (43) Mkazi wa Mbagala rangi tatu, amesema kuwa Kampeni ya mazingira itasaidia sana watu kupata elimu na kufanikiwa kutunza mazingira.

"Naamini mazingira yakisafishwa na kutunzwa vizuri yanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kizazi hiki na kizazi kijacho" amesema Jumanne.

Fatuma Juma Mkazi wa Chamazi, ameeleza kuwa kampeni ya mazingira  inafundisha mazingira yanatakiwa yasafishwe na kutunzwa ili yaendelee kuboresha uhai wa viumbe hai kwa miaka hii ya sasa na miaka ya baadae.

Amesema kuwa mazingira ndio yanayodumisha uhai wa miti na wanyama waishio duniani wakiwemo watu, hivyo ni vizuri tukaendelea na utuzaji wa mazingira yetu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mhe. Makamba amesema kwa lengo la kamapeni ya mazingira ni kuendelea kuelimisha umma ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa.

Mhe. Makamba amesema kuwa wataendelea na kampeni ya utunzaji wa mazingira katika mikoa yote ya Tanzania, jambo ambalo litasaidia kuongeza uwelewa mpana juu ya umuhimu wa kutunza mazingira.

"Tutakuwa tunatumia taasisi mbalimbali katika kutoa elimu kwa jamii pamoja na kutumia mbinu ili kuhakisha elimu inafika kwa jamii na kufanyiwa kazi" amesema Mhe. Makamba.

Katika kampeni ya utunzaji wa mazingira iliyofanyika katika viwanja wa Mbagala Zakhemu, wakazi wa jiji la Dar es Salaam walipata fursa ya kulimishana wenyewe kwa wenyewe pamoja na kupata zawadi mbalimbali ikiwemo majiko ya gesi.

Pia wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwemo Mrisho Mpoto, Roma walipata nafasi ya kutoa burudani kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ambapo kauli mbiu inasema 'Tuza mazingira yakutuze'


Hivyo makala WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA.

yaani makala yote WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wakazi-wa-dar-wampongeza-waziri-makamba.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAKAZI WA DAR WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA."

Post a Comment