title : WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI
kiungo : WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI
WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI
JESHI la polisi mkoa wa Pwani, limewakamata wahamiaji haramu sita ,raia wa nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Aidha mkoa huo umemaliza kusheherekea sikukuu ya Eid Ul Fitr kwa salama na utulivu kwani hakukuwa na tukio lolote la uvunjifu wa amani.
Kamanda wa polisi mkoani humo (ACP) Jonathan Shanna ,alithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao ambao wamekamatwa maeneo ya Msalabani kata ya Dunda wilayani Bagamoyo .
"Katika misako inayoendelea tumefanikiwa kuwakamata raia hao usiku wa kuamkia leo ambao wameingia nchini kinyume na sheria na taratibu zinazotakiwa " alifafanua kamanda Shanna.
Kamanda Shanna aliwataja wahamiaji haramu waliokamatwa kuwa ni Ahamed Mohamed (26) ,Mahad Ahmad (14) ,Abshir Aboulah wote raia wa Somalia .Wengine ni Beyene Abute (25),Abete Eramo (23), Abraham Adoise (24) wote raia wa Ethiopia.
Kwa mujibu wa kamanda huyo alisema ,watuhumiwa wote watawakabidhi idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.Akizungumzia juu ya kumaliza kwa amani sherehe za Eid Ul Fitr alibainisha mkoa huo hauna tukio lolote la uvunjifu wa amani lililojitokeza .
Kamanda Shanna alisema ,licha ya kumaliza salama sikukuu hiyo ,wanaendelea na misako na doria mbalimbali katika mkoa huo ambayo ni endelevu.
Hivyo makala WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI
yaani makala yote WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wahamiaji-haramu-sita-wakamatwa-pwani.html
0 Response to "WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI"
Post a Comment