title : TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU
kiungo : TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU
TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetoa msaada wa taulo za kike katoni 210 zenye thamani ya shilingi milioni tano na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaalum mkoani humo, ambao wanajiandaa na mtihani wa Taifa kwa mwaka 2018.
Akizungumza na viongozi, walimu na wanafunzi wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Bariadi Mjini Bariadi, Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa, Bw. Moses Mbambe amesema msaada huo umetolewa kujibu ombi la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alilolitoa kwa Mamlaka hiyo kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walio kwenye kambi ya Kitaalum mkoani humo ili wawapo kambini wasome kwa utulivu na kujiamini hususani wakati wa hedhi.
“Tunakabidhi taulo hizi za kike kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo ambazo Mkuu Mkoa wa Simiyu alimuomba ili ziweze kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walioko kwenye kambi za kitaaluma katika maeneo mabalimbali hapa mkoani katika kuwawekea mazingira mazuri ya kusoma kuwa utulivu na kujiamini wakati wa siku zao za hedhi” alisema
Aidha, Mbambe ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kuanzisha utaratibu wa kambi za kitaaluma na akawataka wanafunzi kuwa na ndoto, kusoma kwa bidii na kuweka mikakati ya kuwawezesha kufikia ndoto zao; huku akiwaasa kufanya vizuri katika mitihani yao ili kutoa nafasi kwa walio nyuma yao kuwekewa utaratibu endelevu wa kambi za kitaaluma katika kuuwezesha mkoa huo kufanya vizuri kielimu.
Kutoka kulia Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe na Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia Simwanza wakimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka taulo za kike zilizotolewa Mamlaka hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa kidato cha nne zaidi ya 3000 walio katika kambi za kitaaluma mkoani humo, kushoto ni baadhi ya wananfunzi hao wakipokea kwa niaba ya wenzao, katika Shue ya Sekondari Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa saba kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kike walio katika Kambi ya kitaaluma Shule ya Sekondari Bariadi baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa saba kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kike walio katika Kambi ya kitaaluma Shule ya Sekondari Bariadi baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .
Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari Bariadi, Somada, Chenge na Gudui kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi.
Hivyo makala TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU
yaani makala yote TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/tfda-yatoa-msaada-taulo-za-kike-kwa.html
0 Response to "TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU"
Post a Comment