title : SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU
kiungo : SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU
SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
SERIKALI mkoani Mwanza imezindua klabu ya wachangiaji damu wa kundi maalumu (RH Nagative) na kuahidi kuendelea kuhamasisha jamii iweze kuchangia damu itakayosaidia kuokoa maisha ya watu na kuipongeza Taasisi ya The Desk & Chair Foundation kwa mchango wake wa kujitoa kuhamasisha jamii kuchangia damu.
Klabu hiyo ilizinduliwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wachangiaji Damu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Akizungumza baada ya kuzindua klabu hiyo Mongela alisema uhaba wa damu ni changamoto kubwa kwa Mkoa wa Mwanza ambapo mahitaji yake ya damu ni chupa 30,000 na hivyo jamii isisubiri hadi iuguliwe ndugu ndipo ichangie damu.
“Wachangiaji damu waenzie lakini niwapongeze The Desk & Chair Foundation, wamejitoa sana mkoani kwetu na taifa kwa ujumla lakini pia wanafunzi wamekuwa msaada mkubwa kwa kubeba jukumu la kukusanya damu.Hivyo kwa uhaba wa damu mkoani kwetu kila mmoja atambue umuhimu wa kuchangia damu ili wagonjwa waongezwe damu iliyo salama,”alisema Mongela.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary tesha aliyemwalikisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza na wadau wa damu kwenye maadhimisho ya siku ya Wachangiaji Damu jijini humo.
Mfadhili Mkuu wa Kituo cha Damu Salama Kanda ya Ziwa, Mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wachangiaji Damu Duniani iliyofanyika jijini Mwanza kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akichangia damu wakati wa maadhimisho ya Siku ya wachangiaji Damu Duniani wakati wa maadhimisho hayo jana yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure ya Mkoa wa Mwanza, Tesha alimwakilisha Mkuu wa Mkoa John Mongela ambaye alijuwa mgeni rasmi.
Wadau wa damu wakichangia damu kwenye maadhimisho ya Siku ya wachangiaji Damu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya sekou Toure. Picha zote na Baltazar Mashaka
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU
yaani makala yote SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/serikali-kuendelea-kuhamasisha-jamii.html
0 Response to "SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU"
Post a Comment