title : SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO
kiungo : SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO
SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO
JOSEPH MPANGALA -MTWARA
Shirika la msaada wa maendeleao ya Michezo SDA Mkoa wa Mtwara Limefanikiwa kutoa Mafunzo pamoja na Vifaa vya michezo kwa Shule Mbili za Msingi Libobe Pamoja na Sekondari zilizopo Kijiji cha Libobe Kilichopo Wilaya na Mkoa wa Mtwara.
Mafunzo hayo yamelenga Kujenga uwezo kwa wanafunzi hasa wa kike katika maswala ya Afya Kupitia Michezo pamoja na kujua haki zao ili kuweza kujiamini katika kutoa maamuzi mbalimbali ya maisha yao.
Meneja Mradi wa Mradi wa Kuwezesha wasichana Kupaza sauti Unaoendeshwa na SDA Thea Swai amesema Mradi huo unaendeshwa katika kata Tisa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara manispaa kwa lengo la kuelimisha na kujengea Uwezo wa Umuhimu wa Umuhim wa Elim kwa wasichana na Jamii kwa ujumla .
“Lengo kuu la Mradi huu ni kuelimisha na Kujengea Wasichana na Jamii kuhusu Umuhim wa Elimu kwa ujumla juu ya upatikanaji Ushiriki na ufikiwaji wa elim ya msingi na sekondari hasa kwa watoto wakike ambao wamekuwa wahanga wa matatizo ya ufaulu mdogo wanapomaliza elim ya sekondari na wakati mwingine kwa idadi ndogo ya wasichana wanaomaliza shule za sekondari”
Lakini naye Afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmahauri ya Mtwara Vijijini Maisha Mlaponi amewaomba wazazi kuhakikisha wanawajengea Uwezo wa Kijamini wanafunzi ili waweze kufanya Vizuri wawapo darasani.
“Wazazi naombeni Muwasaidie watoto wenu wa Kike waweze kujiamini katika Maisha yao na wakiweza kujiamini hata darasani wataweza kufanya vizuri kwa sababu watakuwa na uwezo wa kuuliza maswali kwa walim na hivyo wataweza kuelewa na kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho’”.
Mkurugenzi wa Shirika la SDA Adolph Kanda akimkabidhi Mwalim wa Shule ya msingi Libobe Mwanaidi Mtanda Vifaa vya Mchezo wa Mpira wa Pete kwa ajili ya kufanyia mazoezi Shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Shirika na Msaada wa Maendeleo ya mischezo SDA Adolph Kanda akinyanyua Juu kuonesha medali walizokabidhiwa wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Libobe mara baada ya Kumaliza mchezo wa mpira wa Miguu.
Kutoka Kulia ni Mratibu wa Mradi Anu Nieminen katikati Mratibu wa Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Mtwara Adelina Ndyamukama pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Paralegal Mkoa wa Mtwara Mullowellah A.Mtendah wakiwa wanajadiliana jambo katika mafunzo yaliyofanyika kwa wanafunzi wa Libobe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mtwara Paralegal Mullowelh A.Mtendah akitoa mafunzo yakisheria kuhusu haki za watoto pamoja na haki za walemavu katika kuhakiksha zinasimamiwa na kutekelezwa na wanakijiji wa Libobe Mkoani Mtwara.
Meneja wa Mradi wa Kuwawezesha wasichana Kupaza sauti Thea Swai akitoa mafunzo ya kujiamini kwa wanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha waweze kupaza sauti katika Kutetea haki Zao.

Hivyo makala SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO
yaani makala yote SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/sda-yakabidhi-vifaa-vya-michezo.html
0 Response to "SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO"
Post a Comment