title : Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti
kiungo : Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti
Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti
Balozi wa Jamhuri ya Ireland Paul Sherlock amepokea maombi ya ushirikiano baina ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na nchi yake yaliyolenga kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti mkoani humo jambo litakalopelekea kuinua kipato cha mkulima wa mkoa wa huo.
Maombi hayo yaliyowasilishwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kwa balozi huyo mapema mwezi huu yalionyesha hali ilivyo ya uzalishaji wa zao hilo kwa sasa, ambapo kati ya hekta za shamba la Alizeti 0.5 hadi 2 huzalisha tani 1.1 badala ya tani 2.5.
“Nimefurahishwa sana na jitihada za Mh. Joachim Wangabo kwa kuona umuhimu wa kutafuta zao mbadala la biashara katika Mkoa wa Rukwa ikiwa ni pamoja na kuinua kulimo cha mkoa na kuinua kipato cha wakulima wadogo na hatimae kuwatafutia namna ya kuongeza viwanda vidogo na kuongeza ajira,” Alisema Balozi Sherlock.
Kwa upande wake Mh. Wangabo amesema kuwa zao la mahindi linazalishwa kwa wingi sana katika mkoa wake na wakulima hulichangamkia hilo zaidi ila bei ikitetereka wakulima hao wanakosa pa kujishika hivyo kwakuwa zao la alizeti ni la pili la kibiashara basi ni vyema kulitafutia mikakati liwe sawa na zao la mahindi ili wananchi wachague.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akipeana mkono na Balozi wa Jamhuri ya Ireland nchini Paul Sherlock muda mfupi baada ya maongezi ya mikakati ya kukuza uzalishaji wa zao la Alizeti Mkoani Rukwa.
Hivyo makala Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti
yaani makala yote Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/rukwa-kushirikiana-na-ireland-kuongeza.html
0 Response to "Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti"
Post a Comment