title : RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU
kiungo : RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU
RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU
Na. VERO IGNATUS ARUSHA
Mkuu wa mka wa Arusha Mrisho Ghambo amefanya mkutano wa siku moja na waandishi wa habari ukiwa na lengo la kuimarisha na kuboresha mahusiano kati ya Serikali na wanahabari.
Katika mkutano huo wa siku moja ambao ni wapili tangia kuingia madarakani umewajumuisha wadau mbalimbali wa Taasisi za serikali mkoani hapa katika kueleza mafanikio changamoto mbalimbali za maendeleo na namna ya kuzitatua.
Katika ufafanuzi zaidi Gambo amesema kuwa asilimia 80%ya mapato mkoani hapo yanatokana na utalii hivyo amewataka wanahabari kuwa makini taarifa ambazo wanaandika wazichuje kabla ya kuzipelea katika jamii."Mfano habari ya mtalii kutekwa, mwandishi unapoaiandika hiyo habari na kuitoa katika vyombo vya habari, itasomwa na inaweza kuleta madhara, kuwaogopesha wageni kutokuja nchini kwaajili ya utalii, kuweni makini tangulizeni uzalendo kwanza"
Amewataka viongozi mkoani hapa Kuwapa ushirikiano wa kutosha waandishi kwani kuna baadhi ya viongozi wanawakimbia waandishi na kuwalazimisha waandike kadri wanavyoona inafaa,amekemea na kuwataka kutoa ushirikiano. RC Gambo amepongeza juu ya jambo la kujiendeleza kielimu kwa waandishi ambapo ameutaka uongozi wa, APC kupeleka data base ili uongozi wa mkoa waone ni namna gani unaweza kuandika andiko kwa wadau mbalimbali kwaajili ya kuwasapoti kielimu.
Gambo amewataka wanahabari mkoani hapo kutokukubali kurubuniwa au kutumiwa na mtu awae yeyote yule ili kuharibu amani badala yake watangulize Uzalendo kwanza kwaajili ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Charles Kwitega akizungumza katika mkutano huo katika Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha AICC Arusha Eliashialia Kaaya.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiendesha mazungumzo pamoja na mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea katika kikao. Cha siku. Moja cha waandishi wa habari pamoja na wadau wa taasisi za serikali mkoani hapo. Picha na Vero Ignatus.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Gabriel Daqarro akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku moja ulioitishwa na mkuu wa mkoa huo. Picha na Vero IgnatusKatibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Charles Kwitega akizungumza katika mkutano huo katika Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha AICC Arusha Eliashialia Kaaya.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU
yaani makala yote RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/rc-gambowaandishi-kuweni-wazalendo-kwa.html
0 Response to "RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU"
Post a Comment