title : POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
kiungo : POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
Na Jeshi la Polisi.
Michezo ya pili ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018) inatarajia kutimua vumbi jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo nchi 14 tayari zimethibitisha kushiriki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Maandalizi ya Michezo hiyo kinachofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili, Mkuu wa Utawala ndani ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Leonard Paul amesema lengo la michezo hiyo kuimarisha ushirikiano na kubadilishana mbinu za kupambana na uhalifu kupitia michezo.
DCP Paul amesema Jeshi la Polisi Tanzania tayari limeanza maandalizi ili kuhakikisha kuwa michezo hiyo inafana na ushindi unabaki hapa nyumbani na ili kufikia lengo hilo wanamichezo hao wanatarajia kuingia kambini hivi karibuni ili wapate muda mrefu wa kujiandaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo hiyo Naibu Kamishna wa Polisi DCP Daniel Nyambabe alisema wadau mbalimbali wanakaribishwa kufadhili michezo hiyo ambapo alizitaja nchi zinazotarajia kushiriki kuwa ni pamoja na Burundi, Comoro, Djibout, DRC Congo, Elitrea, Ethiopia, Kenya , Uganda, Rwanda, Sudan, Sudani kusini, Somalia, Shelisheli na mwenyeji Tanzania.
Mwaka jana michezo hiyo ilifanyika Kampala Uganda na Polisi Tanzania walishika nafasi ya tatu katika ushindi wa jumla na nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwenyeji Uganda na ya pili ilikwenda Kenya.
Mkuu wa Utawala ndani ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Leonard Paul akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa maandalizi ya Michezo ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018). Michezo hiyo inatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 katika Viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku mbili wa maandalizi ya Michezo ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018). Michezo hiyo inatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 katika Viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
Washiriki wa mkutano wa siku mbili wa maandalizi ya Michezo ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018) wakiwa katika picha ya pamoja. Michezo hiyo inatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 katika Viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
Hivyo makala POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
yaani makala yote POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/polisi-tanzania-kuandaa-michezo-ya.html
0 Response to "POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI"
Post a Comment