title : MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 KUKAMILIZA UJENZI WA BARABARA.
kiungo : MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 KUKAMILIZA UJENZI WA BARABARA.
MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 KUKAMILIZA UJENZI WA BARABARA.
MAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Manispaa ya Ilala imeingia makubaliano ya ujenzi wa barabara zenye thamani ya Milioni 39.062 zinazotarajia kujegwa katika Kata ya Tandale, Mburahati pamoja na Mwananyamala.
Akizungumza katika hafla ya kutiliana sahihi ya Mikataba ya Ujenzi baina ya serikali na wakandarasi, Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumjuli amesema kuwa Kampuni ya CRJE East Africa Ltd na China Railway South Group Co. Ltd zimefanikiwa kushinda zabuni katika mradi huo.
Amesema kuwa mradi wa awamu ya tano utatekelezawa na kampuni ya CRJE huku mradi wa sita utajegwa na China Railway Group Co.Ltd.
Kagurumjuli ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hizo itakuwa katika kiwango cha Lami, mifereji, Taa, njia za watembea kwa mguu pamoja na vyoo katika Kata ya Tandale na Mburahati.
" Ujenzi tunatarajia kuanza Juni 4 mwaka huu na kumalizika Augusto mwaka 20I9" amesema Kagurumjuli.
Amefafanua kuwa tayari wakazi wote wa maeneo hayo yamelipwa fidia, hivyo wakandarasi muda wowote kuanzia sasa wanaanza kazi kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta, amesema kuwa serikali itaendelea kuwajali wananchi wake kwa kuhakikisha inaboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara.
Sitta amaeleza kuwa serikali inatumia gharama kubwa katika kujenga mradi wa barabara, hivyo wakandarasi wanapaswa kufanya kazi kwa kiwango kinachostahili.
" Natarajia wakandarasi watafanya kazi kama tulivyokubaliana katika ujenzi wa barabara ambazo zinatarajia kumalizika mwakani" amesema Sitta.
Hata hivyo ameishukuru serikali Kuu pamoja na Ofisi ya Rais kwa kufanikisha mradi huu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happy, amesema kuwa fedha za kutekeleza mradi wa barabara serikali imekopa.
Amesema ni vizuri yake ambayo wamekubaliana katika mkataba yanapaswa kutekelezwa ili kuhakikisha fedha inatumika kama ilivyokusudiwa.
Hivyo makala MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 KUKAMILIZA UJENZI WA BARABARA.
yaani makala yote MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 KUKAMILIZA UJENZI WA BARABARA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 KUKAMILIZA UJENZI WA BARABARA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/manispaa-ya-kinondoni-yaingia-mkataba.html
0 Response to "MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 KUKAMILIZA UJENZI WA BARABARA."
Post a Comment