MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI

MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI
kiungo : MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI

soma pia


MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI

Na Stella Kalinga, Simiyu
Madiwani tisa kati ya 11 wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea Juni 10, 2018 kwenye msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James katika Kijiji cha Kisesa wilayani humo wametolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kupatiwa matibabu ya awali na kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Madiwani hawa walisafirishwa  jana jioni wakisindikizwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, viongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa wilaya ya Meatu na Bariadi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wakizungumza kabla ya kuondoka Uwanja wa ndege wa Mwanza wametoa shukrani kwa madaktari  na wauguzi waliowahudumia toka siku kwanza katika kituo cha Afya cha Mwandoya, Hospitali ya Wilaya ya Meatu, Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu na Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa namna walivyowahudumia hali iliyochangia kuimarisha afya zao.

“Ninashukuru kwa matibabu ya awali niliyopewa Meatu na Bariadi  yamenisadia sana, baada yaajali nilikuwa na maumivu makali sana lakini kutokana na huduma niliyoipata nina nafuu, yamebaki maumivu  ya kifua kwa ndani” alisema Mhe. Pius Machungwa Diwani wa Kata ya Ngh’oboko ambaye pia  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
 Diwani wa Kata ya Itinje wilayani Meatu Mhe.Seni Sitta  Mizumali ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika ajali , kwenye Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu akisaidiwa kuingia kwenye ndege kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wengine wakimsaidia Diwani wa Kata ya Mwamanongu wilayani Meatu Mhe.Emmanuel Sayi Mboje ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kuingia kwenye ndege kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumzana baadhi ya madiwani waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na madiwani sita waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi, madiwani watatu hawapo pichani kutokana hali za kutoruhusu kusimama walikuwa wameshaingizwa kwenye ndege.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na Diwani wa Viti Maalum Consolatha Lushu  katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya diwani huyo na wenzake kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI

yaani makala yote MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/majeruhi-wa-ajali-meatu-wasafirishwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI"

Post a Comment