HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO

HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO
kiungo : HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO

soma pia


HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

RAIS wa Marekani Donald Trump na Kim Jung Un wa Korea  Kaskazini wamekutana katika mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu ambao umefanyika katika Hotel ya Capella katika Kisiwa cha Utalii cha Sentosa, Singapore. 

Trump na Kim Jung Un wamefanya mazungumzo yanayoaminika ni ya kuleta amani na umoja baina ya mataifa hayo mawili.

Wawili hao walikutana kwanza faragha kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa faragha na wakalimani wao lakini baadaye maofisa wa pande zote mbili walijumuika katika mazungumzo hayo.

Awali, Mkutano huo ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa kufurahi na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.

Rais Trump amesema wawili hao walipiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka ya makubaliano.

Imeelezwa wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.

Baadaye walitia saini waraka wa makubaliano ambayo yatawezesha  kurudishwa kwa wafungwa na mateka katika nchi zao.

Katika kuupa umuhimu mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa umoja huo utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliano katika mkutano huo.
''Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu.

"Kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote," amesema Guterres.

Singapore ni nchi ya tatu ambayo Kim Jong-Un ameitembelea tangu alipokuwa Kiongozi mwaka 2011.
Safari yake ya kwanza ilikuwa nchini China Machi na Aprili akawa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kutembelea Korea Kusini ambapo alikutana na Moon Jae-in. 

Na mkutano huo na Trump unatarajia kufungua njia itakayowezesha kuondolewa kwa vikwazo mbalimbali ilivyowekewa nchi yake ya Korea Kaskazini.


Hivyo makala HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO

yaani makala yote HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/hatimaye-rais-trump-kim-jung-un.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO"

Post a Comment