title : Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC
kiungo : Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC
Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ameipongeza Benki ya taifa ya biashara NBC kwa kasi na juhudi za kukuza Uchumi wa Zanzibar.
Akizungumza mkuu wa mkoa wa mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud kwa niaba ya Rais katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort,amesema kuwa pato la Taifa limekuwa likikuwa mwaka hadi mwaka kutoka na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali ikiwemo benki hiyo ya NBC.
Dkt Shein ameipongeza benki hiyo kwa kuonyesha umuhimu kwa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo ya kufutirisha na kutoa huduma nyingine mbali mbali kwa jamii.
Aidha akizungumza katika hafla hiyo ya futari Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya NBC Dk Kassim Hussein amesema kuw kwa huduma za kifedha kisiwani Zanzibar ni kutokana na juhudi bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja wake.
Dk Hussein amesema kuwa mazingira salam yaliopp Zanzibar yanayoimarishwa na viongozi wakuu wa nchi imewezesha benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma za kifedha kwa ufanisi zaidi.
Vile vile amesema kuwa benki hiyo imeanzisha huduma za kibenki kiislam ambayo inatoa huduma za mikopo kwa misingi ya sheria ya kiislamu.
Katika hafla hiyo ya futafi iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein,Mawaziri,Jaji Mkuu,Mufti mkuu wa Zanzibar viongizi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wateja wa benki ya NBC.
Kaimu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya NBC Dk.Kasim Hussein wakati wa kufutu katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki akizungumza kuwa benki hiyo imeshaanzisha huduma ya kibenki ya kiislamu ambayo itatoa huduma za mikopo kwa misingi ya sheria ya Kiislamu.
Raiz wa Zanzibar na Maenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akichukua chakula wakati wa kufuturu futari iliyoandaliwa na na Benki ya NBC,mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Hivyo makala Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC
yaani makala yote Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/dk-shein-kuhudhuria-hafla-ya-futari.html
0 Response to "Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC"
Post a Comment