title : BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE
kiungo : BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE
BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE
Na Agness Francis,Globu ya Jamii.
KIKUNDI cha ngoma cha Bujora Dance kililokwenda Nchini India katika tamasha la michezo ya asili Afrika kimerejea nchini.
Kundi hilo lililofanya vizuri zaidi katika mashindano ya Tulia Traditional Dances Festival 2018 ambao waliibuka kuwa ndio washindi limeifanya Tanzania kuwa kivutio huko nchini India.
Ambapo kundi hilo kutokea mwanza Mei 25 mwaka huu ndio lilianza kufanya kazi hiyo ya michezo asili ya Mtanzania ambapo waliifanya nchi yetu kuwa kivutio katika tamasha la hilo iliyoshirikisha nchi nane lenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kitamaduni.
Kiongozi wa msafara huo Hassan Ngoma amesema kuwa tamasha hilo lililokonga nyoyo za watu wengi sana lilifanyika katika miji mitatu New Delhi, khairagah pamoja na Chandigarh huko nchini India.
Ambapo Usiku wa May 27 heshima nyingine ya Tanzania ilitengenezwa katika mji wa Chandigarh nchini hapo huku kundi hilo la ngoma za asili walionyesha tena uwezo wao katika tamasha hilo.
Ngoma amesema usiku wa Mei 30 ndio walihitimisha kufanya maonyesho yao katika tamasha hilo la wiki ya Afrika ambapo walimalizia kwa kutoa burudani ya uhakika katika mji wa Khairagarh wakiwa ndio waalikwa pekee katika mji huo.
"Imekuwa fursa nzuri kwetu ya kuitangaza tamaduni ya kitanzania kwa nchi mbali mbali lilitoshiriki tamasha la michezo ya asili Afrika" amesema Hassan Ngoma.
Kiongozi wa msafara Hassan Ngoma(katikati) akiwa pamoja na wanakikundi cha Ngoma cha Bujora cha Mkoani Mwanza wakiwa wamewasili kutoka Nchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti.
Kikundi cha Bujora kikiwa kimewasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakitokeaNchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti.
Hivyo makala BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE
yaani makala yote BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/bujora-dance-group-warejea-nchini.html
0 Response to "BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE"
Post a Comment