title : BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI
kiungo : BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI
BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa tatu kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Mil.100, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (wa tatu kulia), kwa ajili ya kusaidia ukarabati wodi ya wagonjwa wa moyo, katika Taasisi hiyo, Muhimbili jijini Dar es Salaam.Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya ya Moyo, Dkt. Tulizo Shemu, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa pamoja na Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Jessica Nyachiro.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza jambo katika mkutano wake na uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ulioambatana na kuchangia fedha kiasi cha sh. mil 100 kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya wagonjwa wa moyo, katika Taasisi hiyo, Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza jambo wakati akitoa taarifa ya Taasisi yake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei aliyeambatana na ujumbe wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Hivyo makala BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI
yaani makala yote BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/benki-ya-crdb-yatoa-sh-mil-100-kusaidia.html
0 Response to "BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI"
Post a Comment