title : ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA
kiungo : ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA
ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA
*Ni baada ya mabasi ya Mashallah, Ngombare kuhamishwa kituo namba 21
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
ABIRIA wanaosafiri kwenda katika mikoa ya Kusini hasa Mkoa wa Lindi na Mtwara, wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa hatua zake za kuhamisha huduma za usafiri wa mabasi ya Kampuni ya Mashalaah kutoka kituo Namba 21 kwenda kituo Namba 48 vilivyopo eneo la Mbagala Jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo ya kuhamishwa kwa mabasi hayo kumesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaotumia mabasi hayo na sasa wanaomba halmashauri hiyo kutafakari upya uamuzi huo.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la kituo namba 21 na baadae katika kituo namba 48 jijini Dar es Salaam, abiria hao walisema kitendo hicho pamoja na mambo mengine, kimekuwa kikiwasababishia baadhi yao kupoteza mizigo na wakati mwingine kulazimika kutumia fedha za ziada kwa ajili ya kukodi piki piki na hata mikokoteni kuyafuata mabasi hayo katika kituo Namba 48, ambacho kipo mbali na neo la Barabara Kuu mahali walipokuwa wakipandia hapo awali.
Abiria hao akiwemo Mustafa Salehe, alisema kubadilishwa kwa utaratibu wa mabasi hayo kutoka kituo namba 21 kwenda kituo namba 48, kumesababisha changamoto kubwa kwa mamia ya abiria hasa wale wanaotumia kituo hicho cha Mbagala, eneo ambalo ndilo linalotumika kama kituo kikuu cha daladala kutoka maeneo mbalimbali ya mji. “Zamani ulikuwa ukishuka hapa kutoka mahali popote ndani ya mji huu, moja kwa moja unaingia katika basi kuendelea na safari yako, lakini kwa sasa inashangaza kuona huduma hiyo imeondolewa tena kwa baadhi ya mabasi, suala linaloleta wasiwasi kuwa pengine kuna mgogoro unaoendelea baina ya uongozi na wamiliki wa mabasi hayo” alisema Salehe.
Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwanakopa Hassan, mbali na kudai kushangazwa na hatua hiyo, alisema hali ya usafiri katika kituo hicho imekuwa ya kutoeleweka kutokana na mkanganyiko unaojitokeza mara kwa mara mahali hapo. “Hapo zamani tulikuwa tunapandia kituo hiki kikubwa cha daladala cha Rangi tatu( kituo namba 21), baadae tukahamishwa tena kwenda huko mitaani(Namba 48),
“Lakini kabla hatujakaa vizuri huduma zikarudishwa tena eneo la mara ya kwanza, na sasa wamezipeleka tena huko huko mitaani, jambo ambalo sisi kama abiria linatuchanganya ikizingatiwa siyo kila mtu mwenyeji wa mji huu” alisema Mwanakopa .Kwa mujibu wa abiria hao, huduma hizo za usafiri zimehamishwa kituo hicho kwa kampuni mbili za mabasi ambazo ni Ngombale pamoja na Mashallah, huku mabasi mengine yakiachwa jambo lililotoa tafsiri kwa abiria hao kuwa pengine linatokana na mgongano wa kimaslahi baina ya watoa huduma hao, uongozi wa manispaa pamoja na wasimamizi wa huduma za usafiri.
Walipotafutwa kuthibitisha suala hilo, Uongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA)ulisema hali hiyo inasababisha manyanyaso kwa abiria hao na unatokana na kiongozi Ofisa mmoja wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke pamoja na kiongozi kutoka Manispaa ya Temeke, na suala hilo wanalifuatilia. “Inashangaza kuona kila siku ni kampuni hizi hizi mbili ndiyo zinayumbishwa pale katika eneo la kutoa huduma, kuna tatizo gani, nini kimejificha..kwa taarifa tulizozipata wapo watu wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, jambo ambalo sisi kama uongozi wa wasafirishaji hatuwezi kulifumbia macho” alisema Katibu Mkuu wa TABOA Enea Mrutu.
Kwa upande wa uongozi wa mabasi hayo umesema kuwa unasikitishwa na hali inayoendelea dhidi yao na kufafanua kwa sasa wanasubiri haki itendeke baada ya kupeleka malalamiko yao maeneo husika huku wakidai kuna baadhi ya maofisa wa halmashauri na polisi kikosi cha usalama barabarani ambao wanawafanyia hujuma za kibiashara.
1: Baadhi ya abiria wakipakia mizigo yao kwenye basi la Mashaalah baada ya kuletwa kwenye mikokoteni kutoka kituo namba 21 kuja kituo namba 48 ambacho kinalalamikiwa na abiria kuwa kimewasababishia usumbufu.
Mmoja wa abiria wa basi la kampuni ya Mashalaah(aliyevaa fulana nyeusi) akitoa malalamiko yake kutokana na adha ambayo wanaipata tangu kuhamishwa kituo namba 21
Mizigo ya abiria ikitolewa kituo cha mabasi namba 21 kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam ikiwa kwenye mkokoteni kwa ajili ya kupelekwa kituo namba 48.
Baadhi ya abiria wa basi la Mashalaah wakiwa wamekaa nje ya ofisini ya basi hizo wakisubiri mizigo yao ipakiwe kwenye mikokoteni ili kufuata basi linakoegesha baada ya kuondolewa kituo namba 21 ambacho ndicho kituo kwa ajili ya abiria wanaokwenda mikoa ya Kusini na kupelekwa kituo namba 48.

Hivyo makala ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA
yaani makala yote ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/abiria-mikoa-ya-kusini-walia-usumbufu.html
0 Response to "ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA"
Post a Comment