title : Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu
kiungo : Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu
Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu
Kuwepo kwa mila potofu katika jamii ya watanzania ni moja na ya jambo ambalo limekuwa ni kikwazo katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi mbalimbali za kijamii katika kupunguza au kutokomeza kabisa matatizo ya kiafya ambayo huwapata watoto wachanga wanaozaliwa na walio na umri chini ya miaka mitano.
Watoto wengi katika rika hilo huwa katika athari ya kuzaliwa au kupata magonjwa ambayo ni kuwa na vichwa maji, pamoja na mgongo wazi, ikiwa ni magonjwa ambayo huweza kuepukwa endapo tu jamii nzima ya watanzania wataweza kupatiwa elimu sahihi ya namna ya kuepuka au kuzuia magonjwa hayo na endapo kutabainika watoto wenye matatizo hayo jamii isiweze kuwaficha kutokana na imani potofu.
Hayo yamebainishwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Bwana Laurent Lemeri Mchome, wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel walipowatembelea watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi pamoja na wazazi/walezi wao waliolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya kuwapa mahitaji mbalimbali ya kijamii kama sehemu ya msaada wao kama wafanyakazi.
“Akiongea baada ya kukabidhiwa msaada huo, kwa niaba ya madaktari na wauguzi wodini hapo Dr Laurent Mchome amesema kila mwaka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) tumekuwa tukitoa matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 350 nchi nzima kupitia kampeni ya watoto wenye vichwa maji na mgongo wazi. Pia tumekuwa tukiweka kambi ya kutibu watoto kila mkoa kwa kila kanda nchini na changamoto kubwa ni kwamba jamii kubwa ya watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusu magoinjwa haya kuwa yanatiwa na watoto hupona kabisa”.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bwana Trieu Thanh Binh na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya Kijamii kwa baadhi wa wauguzi leo wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuwapelekea mahitaji hayo.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bwana Trieu Thanh Binh akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii yenye kwa baadhi wa wauguzi leo wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuwapelekea mahitaji
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Halotel Stella Pius akikabidhi moja ya msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii kwa mmoja wa wazazi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)na kuwapelekea mahitaji hayo.
Hivyo makala Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu
yaani makala yote Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/wito-kwa-jamii-kuondokana-na-mila.html
0 Response to "Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu"
Post a Comment