WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA

WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA
kiungo : WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA

soma pia


WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki kazi za ujenzi wa uwanja mpya wa michezo wilayani Ruangwa kwa kubeba zege na matofali pamoja na wananchi.

Waziri Mkuu ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa, ameshiriki zoezi hilo leo (Ijumaa, Mei 25, 2018) kwenye uwanja huo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Akizungumza na wananchi na viongozi waliojitokeza kushiriki zoezi hilo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi inayoendelea hadi sasa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wana-Ruangwa kwa kurejesha moyo wa kufanya kazi kwa kujitolea.

“Ninawashukuru sana wana-Ruangwa kwa sababu mmeanza kufanya kazi za kujitolea, haya matofali ni matokeo ya kazi yenu, hakuna hata mtu mmoja amelipwa kwa kazi hii. Nimeambiwa yanahitajika matofali 60,000 kwa ajili ya kujenga uzio lakini hadi sasa mmeshafyatua 57,000 na zaidi, ninawashukuru sana,” amesema.

“Nimeambiwa madiwani walipiga kambi ya wiki moja hapa, Umoja wa Vijana wa CCM nao walipiga kambi, UWT walikuja kusomba matofali, watumishi wa Halmashauri nao walipiga kambi, hongereni sana kwa kurejesha moyo wa kujitolea miongoni mwa wananchi,” amesema.

Katika zoezi la leo, walijitokeza wananchi wengi wakiwemo wazee, vijana na watoto. Baadhi ya watoto walikuwa wakibeba tofali moja kwa kushirikiana wawili wawili, watatu watatu hadi wanne.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akichimba msingi wa  jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwana wananchi  kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua nyasi zilizooteshwa kitalaam wakati alipshiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mai mdogo wa Ruangwa, Mei 25, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofali, Bibi Mariam Bakari wakati aliposhiriki katika ujenzi wa  wa msingi wa uwanaja wa michezo unaojengwa na wananchi kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Rungwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wanne kushoto ni  Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofari Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala wakati aliposhiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa na wananchi  katika eneo la Dodoma kwenye  mji mdogo wa Ruangwa,Mei 25, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Bi. Khadija Madoa ambaye ni Mama lishe anayeuza chakula katika mji mdogo wa Ruangwa mkopo usiokuwa na riba wa sh. 200, 000/=  baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo wa unaojengwana wananchi katika eneo la Dodoma, Ruangwa mkoani Lindi Mei 25, 2018. Jumla ya sh. milioni 9 zilitolewa na mfanyabiashara Abdallah Mang'onyola na kutolewa mkopo kwa Mama lishe 42.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkaoani Lindi Mei 25, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa, Mei 25, 2018. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA




Hivyo makala WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA

yaani makala yote WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/waziri-mkuu-ashiriki-ujenzi-wa-uwanja.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA"

Post a Comment