WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI

WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI
kiungo : WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI

soma pia


WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla amekabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili. Magari hayo amewakabidhiwa Wabunge leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma. 
 Wabunge waliokabidhiwa magari hayo ni wa Bunda Vijijini,Boniface Getere ,Itilima,Njalu Silanga ,LongIdo,Dk.Steven Kiruswa,Mbulu Vijijini Flatei Massay,Tanganyika,Moshi Kakoso huku Mbunge wa Ngorongoro,William Ole Nasha yeye hakuweza kufika kutokana na kubanwa na majukumu mengine. 
 Wabunge hao wamepokea kwa niaba ya Halmashauri hizo. Akizungumza kabla ya kuwakabidhi magari hayo,Dk.Kigwangalla amesema jumla ya Halmashauri 6 zinatarajiwa kunufaika na magari hayo. “Tunakabidhi magari ambapo Halmashauri 6 zitanufaika ambayo yanatokana na jitihada za Waheshimiwa Wabunge kutusumbua sana lakini pia utashi wao katika kuunga mkono katika vita dhidi ya ujangili. 
 “Lakini pia magari haya yatatusaidia kwenye doria katika maeneo hayo lakini pia ‘kurespond’ haraka kesi za wanyama waharibifu mfano katika maeneo kama kule Bunda Vijijini katika vijiji vya Mugumu na Mgeta kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana wa wanyamapori na makazi ya watu. “Lakini bahati mbaya Halmashauri zinakuwa hazina usafiri wa ‘Kurespond’ haraka kwenda kuwaondoa wale wanyama hivyo tumeona tuwape gari kama kule kwa wahadzabe,Longido tumeona tuwape magari. 
 “Maeneo kama Itilima hata juzi nilishuhudia kwa masikitiko makubwa watu wawili wakipoteza maisha kwa kuvamiwa na Tembo na Tembo hao walihamia kabisa wakaweka kambi na wamemaliza mazao ya wananchi na wamesababisha vifo. 
 “Tuliona tuzisaidie Halmashauri zetu hivi ili na zenyewe zipate vyombo vya uhakika ili waweze kufika haraka. Waziri huyo amesema sambamba na makakati huo pia Serikali inakusudia kujenga madungu kwa ajili ya kuangalia wanyama tokea wakiwa mbali ndani ya hifadhi. 
 Pia amesema wanatarajia kuweka uzio wa mizinga ya nyuki ili kuzuia wanyama kama Tembo wasitoke katika maeneo ya hifadhi. 
 “Wenzetu hawa wa Tanganyika wao wana msitu mzuri wa Tongwe ambao una nyani na tayari tumeishapitisha msitu wa Tongwe uwe hifadhi na utakuwa chini ya Halmashauri hivyo tumeona tuanze kuwajengea uwezo wa usafiri ili waweze kuuendesha. Dk Kigwangalla ametoa angalizo kwa halmashauri zilizopewa magari kuwa yatumike kwa shughuli za maliasili pekee na sio zingine
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Waandishi wa Habari wakati  akikabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla  akimkabidhi kadi ya gari Mbunge wa jimbo la Bunda, Boniphace Getere katika hafla ya kutoa magari kwa  Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma.
 Baadhi ya Magari  yaliyokikabidhi kwa Wabunge  ya Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili katika hafla iliyofanyika   leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, jijini  Dodoma.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Baadhi ya Wabunge  wakati akikabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla  akimkabidhi kadi ya gari Mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Steven Kiruswa  katika hafla ya kutoa magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma. Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii


Hivyo makala WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI

yaani makala yote WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/waziri-kigwangalla-akabidhi-magari-kwa_12.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI"

Post a Comment