WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL

WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL
kiungo : WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL

soma pia


WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL

Watoto tisa wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanaondoka leo tarehe 28/5/2018 kwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto wataambata na wauguzi pamoja na wazazi wao.

Safari hiyo ya matibabu nchini Israel inahusisha watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka 14 imeratibiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini humo. 

Taasisi yetu inatibu magonjwa mengi ya moyo (kwa asilimia 90) kwa watoto kupitia wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache ambao ni asilimia 10 wanaohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi kuliko uliopo hapa nchini kwa sasa.

Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Aidha tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita na wauguzi wanne ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu. Daktari wetu mmoja na wauguzi wawili bado wanaendelea na masomo nchini humo hii itasaidia kwa siku za mbeleni zaidi ya asalimia 95 ya watoto watatibiwa hapa nchini.

Hili ni kundi la sita la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH) wa kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 56 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Kupitia kipimo hiki mtoto akigundulika kuwa na tatizo la moyo ataweza kupatiwa matibabu kwa wakati na hivyo kuwa na afya njema kama watoto wengine.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
28/05/2018


Hivyo makala WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL

yaani makala yote WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/watoto-tisa-wenye-matatizo-ya-moyo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL"

Post a Comment