title : SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE
kiungo : SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE
SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkoa wa Simiyu umewahakikishia wadau wote wa Nanenane mwaka 2018 upatikanaji wa miundombinu muhimu hususani miundombinu ya maji, umeme na barabara katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo eneo la Nyakabindi Mjini Bariadi, ambapo Mkoa huo utakuwa mwenyeji wa Maonesho hayo Kitaifa mwaka 2018.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini alipokutana na Kamati ya Maadalizi ya Maonesho Nanenane kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambao walitembelea uwanja huo na kupewa eneo ambalo litatumika na wizara hiyo kuonesha shughuli zake.
Sagini amesema viongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na viongozi wa Taasisi nyingine za Serikali wameshafanya mazungumzo na kuweka mipango ya namna kila Taasisi itakavyoshiriki katika kuhakikisha miondombinu ya maji, umeme na barabara inawekwa vizuri ili kufanikisha Maonesho hayo
“Tumeshazungumza na TANESCO na wako tayari kuteremsha Transifoma kwenye eneo lile ili tupate umeme, tumezungumza na Mamlaka za Maji ili tupate fedha za kuchimba kisima kirefu cha maji ya kutosheleza wadau wetu na kuhusu barabara tumezungumza na TANROADS na TARURA, tunatarajia wiki mbili zijazo mambo yatakuwa tofauti pale” alisema Sagini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara ya mifugo na Uvuvi kutembelea Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani humo.
Bi. Merry Yongolo Mratibu wa Maonesho ya Nanenane Wizara ya Mifugo na Uvuvi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara hiyo kutembelea Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya watalaam wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakiendelea na kusafisha eneo lao kwa kutumia greda katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, ikiwa ni maandalizi ya Maonesho hayo yatakayofanyika Kitaifa mkoani humo.
Dkt. Khamis Mkuli kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ziara ya wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara hiyo katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akiwaonesha baadhi ya viongozi na wataalam kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga eneo la Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziawa Mashariki uliopo Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani humo, wakati wa ziara yao walioifanya hivi karibuni mara baada ya kufanya kikao cha pamoja.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE
yaani makala yote SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/simiyu-yawahakikishia-wadau-upatikanaji.html
0 Response to "SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE"
Post a Comment