title : RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO.
kiungo : RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO.
RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amezindua Kamati ya Watu 18 kutoka makundi mbalimbali aliyoiunda kufanya Mapitio kasoro zilizoonekana kwenye Sheria ya Ndoa wakati wa zoezi la kutafuta haki ya Mtoto kisha kutoa mapendekezo kwa lengo la kuweka Ustawi bora wa Mtoto.
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Albert Msando ambae ni wakili wa kujitegemea, Katibu Florah Masue pamoja na wajumbe 16 wakiwemo Wanasheria, Maafisa ustawi wa jamii, Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia na wajumbe kutoka taasisi za kutetea haki ya mtoto ambao watakaofanya uchambuzi wa kina wa kisheria kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo.
"Baada ya kukamilika kwa ripoti hiyo tutaikabidhi kwa Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Afya pamoja na Wizara ya Katiba na sheria kwaajili ya kuwasilishwa Bungeni" amesema
Aidha Makonda amesema miongoni mwa vitu vitakavyoshughulikiwa ni pamoja na mapitio ya Sheria ya mtoto ya mwaka 2009, Muundo wa Mahakama za watoto, kiwango cha fedha ya matunzo ya mtoto kama kinakidhi hali ya sasa, Mamlaka ya Ustawi wa jamii pamoja na kuangalia sheria za kimataifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Albert Msando amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuunda kamati hiyo, na kumhakikishia kuanza kazi maramoja na kufanya kazi kwa uwaminifuna pamoja na kukamilisha majukumu waliyopewa kwa wakati.
"Tutajitahidi kupitia sheria zote zilizopo kwa kuangalia mapungufu yake pamoja na kutoa mapendekezo ili sheria zenye mapungufu ziweze kurekwbishwa" amesema
Hivyo makala RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO.
yaani makala yote RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/rc-makonda-azindua-kamati-ya-kupitia.html
0 Response to "RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO."
Post a Comment