title : JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA
kiungo : JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA
JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akifungua kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote
nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhandisi Mussa Iyombe akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo kufungua kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala za Mikoa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akivishwa beji ya heshima kutokana na utendaji kazi wake.
Wajumbe wa kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dk.Zainab Chaula akizungumza katika kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.
Zulfa Mfinanga na Magdalena Stanley
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Seleman Jafo ametoa siku tano kwa wakurugenzi na waganga wakuu wa halmashauri 10 nchini kutoa maelezo ya kina kwa nini halmashari hizo hazijafika asilimia kumi ya matumizi ya fedha za miradi ya afya.
Jafo ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.
Amesema halmashauri hizo zimeshindwa kutumia fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya afya kama inavyotakiwa ambapo matumizi yake yanaonekana kuwa chini ya kiwango, huku akizitaja halmashauri hizo kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mpimbwe, Mbulu Dc, Songwe, Simanjiro, Mkinga, Mkuranga, Namtumbo, Nzega Dc pamoja na Kilindi.
“Halmasharu hizi zina kila dalili ya kupata hati chafu, naagiza hadi kufika siku ya Jumatano niwe nimepata majibu ya kuridhisha ni kwanini hawajatumia fedha walizopewa kama maelezo yanavyotaka, tukiacha kufanya kazi kwa mazoea tutapata matokeo mazuri, lakini kwa hali hii tusitegemee matokeo mazuri kwa baadhi ya maeneo” Alisema Jafo
Kwa upande mwingine Waziri Jafo aliwaagiza Makatibu Tawala hao kuwaelekeza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwekeana malengo na watumishi wao kwa kuwafanya tathmini ya uwajibikaji kila mwaka ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kazini kwani bado wapo baadhi ya watumishi wanafanya kazi kwa mazoea.
Amesema kuwa iwapo mtumishi wataonekana amefanya kazi chini ya kiwango cha alama 50 kama ni mkuu wa idara atawajibishwa kwa kushushwa cheo, na yule ambaye ataonekana kufanya vizuri zaidi alishauri anastahili kupewa zawadi ya mfanyakazi bora wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani-Mei Mosi.
Aidha Waziri Jafo amesema kwa sasa kipaumbele cha utoaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo zitatolewa kwa kuzingatia kipimo cha matokeo mazuri kwa halmashauri husika, kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza uwajibikaji.
Wakati huo huo Waziri huyo aliagiza halmashauri zote nchini kuweka mfumo wa matumizi ya mfuko wa afya ya jamii wa CHF iliyoboreshwa sambamba ya kuhimiza matumizi ya ukusanyaji wa mapato wa njia ya kimtandao ili kuepuka upotevu wa fedha za serikali.
Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo Mratibu wa mfuko wa afya ya jamii TAMISEMI, Nkinda Shekalaghe amesema kuwa hadi sasa mfuko huo haujafikia lengo lililowekwa na serikali la kuunganisha wananchi kwa asilimia 30 hadi kufikia mwaka 2015, kwani kwa mwaka 2016/2017 wamefikia asilimia 24.
Alitaja baadhi ya changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni pamoja na utayari wa wananchi kujiunga na mfuko, huduma duni za afya, kutokuwepo kwa mfumo rasmi wa utoaji wa taarifa pamoja na kiwango kidogo cha uchangiaji ambapo amesema tayai wameshachukua hatua mbalimba katika kukabiliana na changamoto hizo.
Hivyo makala JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA
yaani makala yote JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/jafo-atoa-siku-tano-kwa-halmashauri-10.html
0 Response to "JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA"
Post a Comment