title : RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI
kiungo : RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI
RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameuagiza uongozi wa wilaya ya Gairo na mkoa wetu kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wa shule msingi mpaka sekondani wanapatiwa chakula mashuleni. Kauli hiyo ameitoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika Ufunguzi wa madarasa ya shule ya sekondari Chagongwe katika ziara yake kwa siku ya tatu Wilayani Gairo kukagua miradi ya maendeleo.
Ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Gairo kujiwekea mpango kazi ili kuwawezesha watoto wote kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari wanapatiwa chakula cha mchana na kuwawezesha waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
"Watoto wa shule za Morogoro kutokula chakula mashuleni ni aibu, sitaki kabisa kusikia hili suala watoto kunyimwa chakula, naomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo, upitishe azimio kwenye baraza na shule ambayo hawatatoa chakula shuleni wachukuliwe hatua uongozi wa eneo hilo," amesema Dkt. Kebwe.
"Mkoa wetu unaongozwa kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha sasa inakuwaje watoto wetu tuwanyime chakula, tutakosa matokeo mazuri," amesema.Aidha amesema kuwa mtoto anatakiwa kula chakula mara mbili ya mtu mzima, unapomnyima chakula hata ukuaji wake unakuwa hafifu... "Ubongo unatakiwa kupata chakula gram 6 za grucose" Amesema kuwa kukosekana kwa chakula shuleni kumekuwa kukichangia matokeo mabaya kwa wanafunzi bila kujali ni shule ya msingi au sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua majengo ya shule ya Chagongwe wakati wa ziaya yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (wa pili kushoto) wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kumaliza ufunguzi wa majengo ya shule ya sekondari Chagongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chagongwe waliojitokeza kumpokea wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Gairo na vitongoji vyake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua vyoo vya hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.
Hivyo makala RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI
yaani makala yote RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/rc-dkt-kebwe-ataka-wanafunzi-wote-wa.html
0 Response to "RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI"
Post a Comment