title : MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI
kiungo : MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI
MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI
Na Mdau wa blog ya jamii
Japokuwa mvua zinaendelea kunyesha, zikiwa zinaweza kuleta madhara makubwa katika barabara mbali mbali jijini Dar es Salaam na nchini kwa Ujumla lakini zipo barabara zinaweza kuokolewa iwapo watendaji husika watafanya kazi zao kwa weledi na bila kusukumwa na mamlaka za juu.
Napenda kutolea mfano barabara ya kutoka Tabata Mwananchi karibu kabisa na ofisi za gazeti la Mwananchi kuelekea Tabata Kisiwani, barabara hiyo imekatwa na maji yaliyoshindwa kupita katika matundu ya Daraja ambayo yameziba hiyo yakaamua kutafuta njia mbadala ya kupitia.
Matundu hayo hayajaziba leo wala jana, yemeziba tangu mvua za awali, na mvua hizo zilikuwa zikisimama hata kwa wiki moja lakini hakuna jitihada zilizochukuliwa na wahusika kuzibua matundu hayo ili kuruhusu maji yapite na kutokuharibu tena barabara.
Unaweza kujiuliza, hivi kipindi mvua zinasimama mamlaka husika hazioni umuhimu wa kuzibua milango ya daraja hilo?, Je hawaoni mateso tunayoyapata wakazi wa Tabata Kisiwani? Je hawajui kuwa kukosekana kwa mawasiliano kati ya wakazi wa Tabata Kisiwani na sehemu zingine ni hatari kubwa hata kwa wagonjwa na akina mama wajawazito pale inapotokea dharura? Je wanataka hadi kiongozi wa juu ili awape maelekezo? na kama wanajua je wanataka kupata nini baada hiyo barabara kuharibika?
Mvua ya leo ndio imekata kabisa barabara nakufanya magari yashindwe kupita huku ile barabara ya kutokea upande wa Tabata Kimanga nayo haipitiki kwakuwa Makalavati yaliyowekwa yameliwa na maji hiasi cha magari kushindwa kupita, kwa ujumla hali si shwari kabisa.
Naziomba mamlaka zinazohusika pamoja na uongozi wa Tabata Kisiwani kuliona hili kama dharura, ili wakazi wa Tabata kisiwani na sisi tujione kama watanzania huru na wenye kustahili kuhudumiwa na watu wenye kupata malipo yanayotokana na kodi zetu, pia naiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuingilia kati suala hili ili kunusuru maisha ya wanatabata Kisiwani ili dharura itakapotokea tuweze kujitete kwa haraka.
Muonekano wa Daraja la Tabara Mwananchi kuelekea Tabara Kisiwani lililovyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha baada ya maji kushindwa kupita kwenye matundu ya daraja hilo na kupita juu.
Muonekano wa Barabara ya kuelekea Tabata Kisiwani kutoka Tabata Mwananchi maji yakiwa yamejaa barabarani baada ya maji wengi kushidwa kupita katika matundu ya daraja lililopo katika barabara hiyo.
Hivyo makala MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI
yaani makala yote MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mvua-yakata-daraja-la-tabata-kisiwani.html
0 Response to "MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI"
Post a Comment